Watu wanaofanya vitu vya tofauti siyo kwamba ni watu ambao wameshuka kutoka mbinguni. Siyo watu ambao wana vitu vya kipekee kukuzidi wewe. Siyo watu ambao wana elimu kubwa kulliko wewe. Isipokuwa ni kuwa wana sifa moja kubwa ambayo inawatofautisha wao na wewe.
Na sifa hii siyo nyingine, bali ni sifa ya kuamua kufanya jambo na kuhakikisha kwamba wanalifanya bila ya kurudi nyuma.
Hii ni sifa ambayo na wewe unapaswa kuwa nayo pia rafiki yangu.
Kuazia leo hii fahamika kama mtu ambaye akiamua kufanya jambo analifanya kweli.
Na kwa sababu ninataka ufahamike hivyo kuanzia leo hii. Nataka uanze kuchukua hatu akuanzia sasa hivi.
Ebu sasa hivi andika chini jambo ambalo unaamua kufanyia kazi kuanzia leo hii.
Kisha nenda kalifanyie kazi kuanzia leo hii.
Lifanyie kazi kila siku kwa siku zijazo mfululizo bila kuacha.
Jipe walau changamoto ya kufanya hilo jambo kwa siku 100 zijazo bila ya kuacha. Ukiweza kufanya hili jambo kwa siku hizi 100 bila kuacha, ni wazi kuwa utakuwa umeweza kujijengea nidhamu kubwa sana. lakini pia utakuwa umejenga njia nzuri yaw ewe kuweza kulifanya hilo jambo.
Na baada ya hapo utakuwa hauzuiliki wala kurudi nyuma hata kidogo
Chukua hatua leo hii
Kila la kheri