Rafiki yangu wa ukweli, siku ya leo Ningependa nikwambie vitu saba unavyopaswa KUZINGATIA pale unapokuwa na miadi na watu.
Kwenye ulimwengu wa Biashara, miadi Ni jambo ambalo haliepukiki. Utahitaji kukutana na Wateja. Utahitaji kukutana na wasambazaji, utahitaji kukutana na washirika, utahitaji kukutana na wafanyakazi na wengineo wengi…
Sasa yafuatayo ni mambo saba ya kuzingatia
Kwanza. Unapokuwa na miadi na watu hakikisha kwamba unawahi kwenye miadi hiyo. Ikitokea kwamba una changamoto inayokuzuia wewe kufika eneo husika kwa wakati, basi wajulishe wahusika.
Pili, unapokutana na watu usigawe umakini wako. NGUVU zako na Akili Yako yote iwe kwenye hiyo miadi.
Tatu, usitumie simu Wala kifaa kingine wakati unaongea na watu.
Nne, hakikisha unakuwa na kalamu na karatasi na andika yale ambayo wengine wanaongea. Chukua notsi. Hii itaonesha namna ulivyo makini kwenye kufanyia Kazi majukumu yako.
Tano, usiingilie Kati mazungumzo ya mtu. Mwachie MTU nafasi ya kuongea mpaka mwisho Kisha ndiyo wewe uingilie kati.
Sita, sikiliza umakini anavyosema mwingine. Haipendezi kuona kwamba mtu fulani anasema jambo fulani Tena kwa namna ya kueleweka halafu wewe unakazana Kuuliza. Hivi umesemaje hapo?
Saba, vaa vizuri ili kuendana na mkutano husika.
Rafiki yangu, hayo ndiyo mabo saba ya kuzingatia pale unapokuwa na miadi. Nikutakie wakati mwema rafiki yangu wa ukweli
Jinsi Ya Kufanya Na Kukamilisha Majukumu Yako Kwa Wakati
Ni Mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
2 responses to “Vitu Saba vya KUZINGATIA unapokuwa na miadi na watu”
Nimependezwa nayo sana nitakuwa nafanya hivyo hongera sana kaka GODIUS
mzuri hii ragiki somo limeeleweka