Wewe unapenda kitu gani?


Kati ya vitu vyote, nilipenda vitabu zaidi– Nikola Tesla

Wewe unapenda kitu gani? Nadhani hili ni swali ambalo ukiuliza kwa vijana kama sisi wa siku hizi utapata majibu ya ajabu Sana.

Kama unaweza kuvumilia *pressure,* Basi uliza hilo swali. Ila Kama una *pressure* ya haraka basi usiliuze labda Kama umechoka kula ugali. Hahaha

Nakwambia hivyo, kwa sababu majibu utakayopata kutokana na swali Hilo yatakusikitisha sana.

Mimi sitataja majibu  utakayopata, hivyo kaulize mwenyewe…..

Utagundua mwanzoni nimeanza na nukuu ya Nikola Tesla ananasema Kati ya vitu vyote, vitabu ndivyo nilipenda zaidi.

Sijajua wewe upande wako vipi.

Leo nimeona nikusisitize zaidi huu ya umuhimu wa vitabu. Vitabu ni vya muhimu Sana kwenye maisha. Nakumbuka siku za nyuma niliwahi KUANDIKA kitabu kizima kinachoeleza NGUVU KUBWA iliyo kwenye Kusoma vitabu na jinsi ya kuitumia hiyo NGUVU kufanya makubwa.

Nashauri na wewe usome hiki kitabu maana kina Mambo mengi mazuri sana ndani yake ambayo yatakunufaisha na wewe. Na ubora ni kwamba unaweza kukipata bure hapa

Kwa kuwa vitabu vina Mambo mengi mazuri. Leo nataka nikwambie kwamba vitabu vina uwezo wa kukutoa kwenye ukilaza kuwa gwiji. Nikola Tesla ambaye nimeanza kwa kutoa nukuu yake hapo mwanzoni, alikuwa gwiji wa Aina yake.

Alifanya Mambo mengi mazuri kwenye ulimwengu wa ugunduzi. Ni mmoja wa watu wanaoaminika kwamba waligundua redio.

Lakini ukifuatilia nyuma yake unakuta kwamba alikuwa anapenda kusoma vitabu. Sijajua Hilo linakuwaje, Ila kila Mara ukifuatilia historia za watu waliofanya MAKUBWA, Kati ya Mambo mengi ambayo najifunza Kutoka kwa hao watu ni kusoma vitabu.

Ninapoandika hapa nipo nasoma historia ya Mkurugenzi maarufu wa kampuni GE. Jack Welch, nadhani ukitafua Google wakurugenzi Bora wa nyakati zote, Ni lazima Jina la huyu jamaa ulikute.

Lakini kinachonishangaza ni kwamba pamoja na mengine mazuri ambayo alifanya ila bado alikuwa anapenda kusoma vitabu.

Hivyo, nadhani usomaji wa vitabu, unabaki kuwa ni moja ya jambo muhimu sana kwenye ulimwengu wa leo. Yaani, unabaki kuwa ni jambo la muhimu mno.

Kati ya vitu vyote ambavyo utafanya, basi hakikisha kwamba unasoma na vitabu pia. Vitabu Ni muhimu Sana.

Tenga muda hata kama Ni kidogo kuhakikisha unasoma vitabu.

Pakua kitabu Cha bure hapa ili uweze kukisoma zaidi

Kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X