Fanya kitu kimoja kila siku ambacho kinakuogopesha. Fanya kitu hata kama ni kidogo. VItu vidogo mwisho wa siku ndyo huwa vinaleta matokeo na mafanikio makubwa sana. Kuna watu wanafikiria kuwa na mtaji mkubwa wa kuanzisha biashara. Kuna watu wanafirikia juu ya kuja kuwa mabilionea.
Hilo lengo ukiliangalia ni lengo kubwa sana. Lakini sasa kulifanyia kazi kwenye uhalisia, ni kazi.
Ndiyo maana unahitaji kulifanyia kazi hata kama ni kidogokidogo . Pata picha kila siku ukifanya jambo moja dogo, tena ukalifanya kwa mwendelezo na bilakuacha, ni wazi kuwa baada ya muda utakuwa umeweza kufanya makubwa.
Mfano, kama kila siku ukiweka akiba, ni wazi kuwa akiba hii kidogokidogo, baada ya muda itakuwa imeweza kuwa akiba kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria.