Tumezindua kitabu kipya! Haya hapa ni mambo ya msingi sana unayopaswa kufahamu kuhusu hiki kitabu


Rafiki yangu mpendwa, Salaam
Moja ya kitu ambacho huwa kinanipa furaha kubwa ni pale ambapo huwa naandika kitabu, na kukikamilisha. Ni vigumu sana kueleza kwa UNDANI mchakato wote wa kuandika kitabu kwa ukamilifu. Ila furaha ile unayoipata baada ya kumaliza kuandika kitabu, ni furaha isiyo na kifani! Hivi unaijua furaha isiyo na kifani kweli……Hahaha

Enewei, leo tarehe 21/4/2021 ni moja ya siku kama hizo.
Ni siku ambapo nina furaha kubwa kutambulisha kwako kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. NA KWA NINI UNAHITAJI KUMALIZA KILE ULICHOANZA.
Kitabu hiki kinapatikana katika mfumo wa nakala ngumu na nakala laini. Na utatumiwa popote pale utakapokuwa duniani.

Labda kwanza tujiulize unaenda kujifunza nini kwenye hiki kitabu na kwanini unapaswa kununua hiki kitabu?
Kama kichwa cha kitabu kinavyosema. Kwenye hiki kitabu unaenda kujifunza nguvu ya kuchukua hatua ya kwanza. Lakini siyo tu kwamba tutaishia kukuonesha wewe nguvu ya kuchukua hatua ya kwanza, bali tutaona kwa nini haswa unapaswa kumaliza kile unachopanga.

Watu wengi sana huwa wanakuwa na ndoto kubwa za kuanzisha na kufanyia vitu. Ila kiuhalisia huwa hawafanyii kazi hivyo vitu. Hivyo, mwisho wa siku huwa wanaendelea kuwa na ndoto kubwa ambazo huwa hawazifanyii kazi.

Unakuta mtu aliyekuwa na ndoto ya kuandika kitabu, ni mwaka wa saba ila hajaandika.
Unakuta mtu alikuwa anasema kwamba ataanzisha biashara tangu mwaka 2010 mpaka leo hii bado anasema tu kwamba ataanzisha biashara.
Unakuta mtu alikuwa anasema kwamba atawekeza au atamfungulia mwanae akaunti, tangu amezaliwa mpaka leo hii mtoto anaelekea kuanza shule, akaunti haijafunguliwa.
Sasa kwenye hiki kitabu tunaenda kuona NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA.

Lakini haitoshi tu kuchukua hatua ya kwanza.

Kumaliza kile ulichoanza ni jambo la msingi na sekondari kabisa. Hivyo hatuishia tu kuona kwamba unapaswa kuanza kufanyia kazi vitu. Bali unapaswa kumaliza kile ulichoanza. Yaani, ukifanyie kazi mwanzo mpaka mwisho.

Siyo uanze kuweka akiba leo. Kesho uache
Siyo uanze kufuga kuku leo, kesho ndiyo tukukute umeanza kulima tikiti, kesho kutwa tukukute umeagiza mzigo china, na siku nyingine tukukute umeanza kuwekeza kwenye cryptocurencies.

Kumbe kwa mantiki hiyo ni kwamba, unapaswa kuanza. Lakini siyo tu kuanza, bali kabisa kuhakikisha umekamilisha kile ulichoanza.

hiki kitabu ni mwongozo. Na ni mwongozo unaopaswa kuufuata.
Kama nakuona vile kitakavyokusaidia kuondokana na lile tatizo lako ambalo limekuwa linakusumbua la kukosa mtaji. ANZA.
Umekuwa unahofia kuongea mbelea ya watu. ANZA, KUJENGA UWEZO WAKO WA KUONGEA MBELE YA WATU.
Umekuwa unatata kuweka akiba. ANZA tena leo hii.
Umekuwa unatamani sana kusoma vitabu. Unasubiri nini. ANZA
Umekuwa unataka kufanya kitu gani….ANZA.

Kitabu sasa kipo tayari. Ni juu yako sasa kuchukua hatua ya kwanza ya kupata kitabu hiki.
Kisha baada ya KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. Utapaswa kusoma kitabu hiki na kukimaliza mpaka mwisho. Hapo utakuwa umeanza vizuri kwenye NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA.

Njoo ujipatie nakala yako siku ya leo rafiki yangu
Nakala ngumu yakitabu ni 20,000/- utaongeza 5,000 ya kutumiwa.
Na nakala laini ni 10,000/-

Ila siku ya leo nina ofa.
Kama utachukua nakala laini softcopy na kulipia siku ya leo. BADALA YA KULIPIA 10,000/- unaenda kupata hiki kitabu kwa 7,000/-

Hii ni ofa ya IDDI na itadumu kwenye hiki kipindi cha EID tu. Hivyo, itaduu mpaka tarehe 25. Baada ya hapo, hutaweza kupata hiki kitabu kwa hiyo bei.
Cha kufanya sasa hivi ni kitu kimoja tu. Wasiliana na 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

ViTU VYA NYONGEZA UTAKAVYOPATA ENDAPO UTACHUKUA KITABU HIKI LEO HII
Kwanza, utapata usimamizi wangu wa karibu wa siku 30. Utachagua kitu chochote ambacho umekuwa unatamani kufanya. Halafu utaniambia na nitakufuatilia kwa siku 30 mfululizo kuona mwnendo wako na namna unavyokifanyia kazi.
Pia, utapewa zawadi ya kitabu cha NGUVU YA KUWEKA MALENGO.
Njoo upate nguvu ya KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. Ili uweze kujifunza NGUVU LIYOLALA kwenye kuchukua hatua ya kwanza.
Lipia 7,000/ sasa kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Lipia sasa upate kitabu chako.

NB: Hardcopy haina ofa kwa sasa hivi.
Ila softcopy, unaipata kwa 7,000 badala ya 10,000

Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
MOROGORO


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X