Usifanye Kosa Hili Unapotaka Kufanya Uwekezaji


Hongera sana Kwa siku hii ya kipekee rafiki yangu.
Nadhani unajua ni Kwa Namba Gani nimekuwa nakusisitiza kufanya uwekezaji.

Wakati mwingine unaweza kusikia watu wakiongelea Kuhusu uwekezaji ukaona nguvu hii iliyolala kwenye uwekezaji, basi ukaamua kwamba na wewe utaenda kuwekeza. Lakini sehemu yako ya kukimbilia ikawa ni kupata mkopo.

Rafiki yangu, ninachotaka kukwambia siku ya Leo ni kuwa usikope Kwa ajili ya kwenda kuwekeza. Iwe ni Kwa ajili ya Kununua hisa, hatifungani au vipande.

Badala ya wewe kukopa Kwa ajili ya hivi vitu, fanya hivi:
Anza kuwekeza kidogokidogo
Hata kama ni kiasi kidogo sana.
Anza kufanya uwekezaji Sasa.
Huu uwekezaji utakufaa sana Kwa siku zijazo.

Unajua Kwa Nini nakwambia usikope Kwa ajili ya kwenda kuwekeza?
Nakwambia usikope Kwa ajili ya kwenda kuwekeza Kwa sababu mrejesho unaoupata kutoka kwenye uwekezaji wako, unaweza kuwa ni mdogo kuliko hata riba unayopata. Hivyo kitu hiki kikasababisha wewe ushindwe kulipa mkopo wako Kwa kutumia uwekezaji uliofanya. Badala yake ukalazimika kutumia vyanzo vingine kulipa mkopo.

Hivyo basi, badala ya wewe kukopa. Kuwa tayari kuanza kuwekeza kidogokidogo. Wekeza hata kama siyo kiasi kikubwa. Nakuhakikishoa hiki kiasi baada ya muda kitakuwa kikubwa kuliko unavyofikiri.

Muda pekee unapaswa kukopa Kwa ajili ya kufanya uwekezaji
Kama kweli ukalazimika kukopa Kwa ajili ya kuwekeza. Basi muda pekee unapaswa kukopa Kwa ajili ya kufanya uwekezaji ni pale unapokuwa unakopa Kwa ajili ya kuendesha maisha.
Kama unakopa Hela ya kula. Kitu ambacho haupaswi kuwa unafanya
Kama unakopa Kwa ajili ya kuendesha maisha yako ya kila siku, basi hakikisha kwamba kwenye kukopa Kwako. Unakopa Kwa ajili ya kufanya uwekezaji pia. Kwenye kile kiasi ulichokopa, toa kiasi kidogo, Kisha kiwekeze.

Kila la kheri.


One response to “Usifanye Kosa Hili Unapotaka Kufanya Uwekezaji”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X