Huyu Ndiye Robert Kiyosaki Na Haya Ni Mambo 20+ Ya Kujifunza Kutoka Kwake


Robert Kiyosaki ni mfanyabiashara, mwekezaji, na mwandishi wa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” Kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu ambavyo vimeuza sana na watu wengi wamekisoma kikiwaletea matokeo makubwa

Alizaliwa Aprili 8, 1947, huko Hawaii, na alikulia katika familia ya maskini ambapo baba yake alikuwa mwalimu. Wakati kiyosaki anakua, alipata kujifunza kutoka kwa baba zake wawili, baba Tajiri ambaye Kiyosaki anasema kwamba huyu alikuwa ni baba wa rafiki yake Mike.

N baba maskini ambaye Kiyosaki anasema kwamba huyu alikuwa baba yake mzazi.

 1. Matajiri hawafanyii kazi kwa pesa bali wanaifanya pesa iwafanyie kazi.
 2. Kosa kubwa watu hufanya ni kufanya ajira kuwa chanzo pekee cha kipato ambacho wanakitegemea mara zote.
 3. Usiogope kuchukua hatua za hatari; kushindwa ni sehemu ya mchakato wa kujifunza.
 4. Huwezi kupata utajiri kwa kumfanyia kazi mtu mwingine; unahitaji kuwa na biashara yako mwenyewe.
 5. Ili kufanikiwa katika biashara, unahitaji kuwa na elimu thabiti ya kifedha.
 6. Elimu ya fedha haijifundishi shuleni; unahitaji kuitafuta mwenyewe.
 7. Matajiri huweka nguvu kwenye rasilimali ambazo huleta kipato zaidi kwao, maskini huweka nguvu kwenye vitu ambavyo vinatoa fedha mfukoni mwao. Chagua kwa usahihi
 8. Kitu kingine Robert Kiyosaki anasema kwamba watu huchanganya kati ya mali na vitu vingine ambavyo siyo mali. Kiufupi ni kwamba mali zinapaswa kuwa zinaingiza fedha mfukoni mwako, na kitu kingine ambacho hakiingizi mali mfukoni mwako basi siyo mali.
 9. Mali isiyohamishika ni uwekezaji bora ambao unaweza kuufanya, kwa sababu hutoa mtiririko wa pesa na huongezeka kwa thamani.
 10. Wakati bora wa kuwekeza katika mali isiyohamishika ni wakati ambapo soko linashuka, wakati bei ziko chini.
 11. Kuwekeza katika hisa kuna hatari zake maana unategemea utendaji wa kampuni.
 12. Usiweke mayai yako yote katika kikapu kimoja; tawanyauwekezaji wako.
 13. Njia bora ya kupunguza hatari yako ni kujifunza kuhusu uwekezaji.
 14. Usisubiri kuwekeza mpaka uwe na pesa za kutosha; anza kidogo na uachilie faida ya kuongezeka kwa mtaji wako.
 15. Jifunze Zaidi kwa kupata kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA hapa
 16. Kuwa makini na matumizi yako; epuka kutumia pesa yako kwa vitu visivyokuwa na maana.
 17. Usisubiri mpaka uwe tajiri kuwa na furaha; furaha inatokana na maisha yako ya kila siku.
 18. Kuwa na mtazamo wa muda mrefu; fikiria jinsi uwekezaji wako utakavyokufaidi siku za usoni.
 19. Jua jinsi ya kuendesha biashara yako vizuri, na jifunze kutoka kwa wataalamu waliofanikiwa.
 20. Usidharau kazi ndogo ndogo; kazi hizo zinaweza kukupa ujuzi na uzoefu unaohitajika kufanikiwa.
 21. Usijaribu kupata utajiri kwa njia za mkato au za hila.
 22. Jenga mtandao wa watu wenye mafanikio na ambao wanaweza kukusaidia kufanikiwa.
 23. Kuwa mvumilivu na usikate tamaa katika safari yako ya kufanikiwa.
 24. Jifunze kutoka kwa wataalamu wengine; soma vitabu na ushiriki katika mafunzo na semina.
 25. Kumbuka kwamba kila mtu ana njia yake ya kufanikiwa; weka malengo yako na fanya kazi kwa bidii.

Hayo rafiki yangu ndiyo baadhi ya mambo ya kujifunza kutoka kwa Robert Kiyosaki mwenyewe, hata hivyo, nahsauri usome vitabu vyake. Utajifunza mengi kutoka kwake. Lakini kama ilivyo kawaida yetu, kujifunza pekee haitoshi, unahitaji kufanyia kazi haya unayojifunza.Kama wanavyosema wahenga kuwa utamu wangoma sharti uingie ucheze. Hivyo hivyo kwenye kufanyia kazi yale unayojifunza pia.

Hivyo basi, nikusihi kitu kimoja tu, baada ya wewe kuwa umesoma hapa, chukua walau kitu kimoja kutoka hapa, kisha anza kukifanyia kazi. Hiki kitu ndicho kitakachokufanya wewe uweze kufanya makubwa na hatimaye uweze ufika mbali sana.

Kupata mafunzo zaidi kutoka kwetu hakikisha kwamba umejaza taarifa zako hapa chini


One response to “Huyu Ndiye Robert Kiyosaki Na Haya Ni Mambo 20+ Ya Kujifunza Kutoka Kwake”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X