Mrejesho Wa Semina Ya Kufanya Makubwa 2023


Habari ya Leo rafiki yangu .
Utakumbuka kuwa kwa siku zanyuma nilikuwa nikikutaarifu kuhusiana na semina ya KUFANYA MAKUBWA MWAKA 2023. Semina hiyo iliweza kufanyika kwa mafanikio makubwa siku ya JUZI kwenye hoteli ya ANTIQUA LEGACY iliyopo hapa mjini MOROGORO.

Nimeona nikupe mrejesho kwa ufupi ili hata wewe ambaye hukuwepo uweze kupata picha ya kilichofanyika na pengine ujiandae kwa ajlil ya semina itakayofanyika mwakani.

1. SEMINA ilienda vizuri. Ilianza saa mbili asubuhi na kukamilika jioni saa 12 jioni.

2. Mada ziliwasilishwa vizuri. Mimi niliwashirisha Kuhusu NAMNA YA KUWEKA MALENGO MAKUBWA NA KUYAFIKIA.

Kwenye hili niliongelea zaidi malengo ya FEDHA na MWISHO nilimtaka Kila Mmoja KUWEKA lengo la kuongeza Kipato mara 2 ndani ya mwaka Mmoja.

Hili ni lengo ambalo kila MMOJA atalifanyia KAZI Kwa mwaka mzima unaofuata huku akipata usimamizi wa karibu kutoka kwangu..

2. Bilionea Alfred Mwanyika, aliongelea Kuhusu uwezo wa KUANZISHA na KUKUZA BIASHARA
Presentation yake ilikuwa nzuri sana.

3. Bilionea Martin Tindwa aliongelea Kuhusu KUJILIPA MWENYEWE KWANZA.
Akizungumzia SABABU kadhaa Kwa Nini kila Mmoja anapaswa kujilipa mwenyewe.

4. Nilimalizia Kwa kuongelea UWEKEZAJI KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE na kutoa Mwongozo ambao tutaufanyia KAZI Kwa mwaka Mmoja unaofuata.

5. Nilipata muda wa kuongea na Kila mshiriki. Na Kila Mmoja alitoka na Kitu ambacho tulikubaliana anaenda kufanyia KAZI Kwa msimamo Kwa mwaka Mmoja ujao.
6. Tulikubaliana na kila mshiriki kuwa nitamtembelea kwenye eneo lake la biashara ndani ya huu na kabla ya semina inayofuata.

7. Tunaenda kuwa na programu endelevu ya kumfuatilia kila mmoja kwa ukaribu kwa mwaka mmoja ujao. Programu hii ya KUONGEZA KIPATO MARA 2 ZAIDI itakuwa ikitoa usimamizi wa karibu kwa kila mmoja. Na ukweli ni kuwa programu hii imeshaanza.

6. Mambo mengine kama chakula na breakfast yalienda vizuri pia

Huo ndiyo mrejesho WA SEMINA. Huo ndiyo mrejesho wa semina kwa ufupi.
Kama hukupata kuhudhuria semina hii bado unaweza kupata mafunzo haya ya semina kwa kuwasiliana 075584839
utapata mfunzo ya semna kwa njia ya video. Gharama yake ni 50,000/-
Karibu sana


3 responses to “Mrejesho Wa Semina Ya Kufanya Makubwa 2023”

  1. Hongerenisana kwa semina nzuri, kiukweli kuna mambo hauwezi kuyafanya bila kuyafahamu kwa undani na kuelekezwa na hauwezi kuyafanya kwa sababuya hofu na roho ya kusitasita na pengine unakuwa kama umenasa mahali ambapo huwezi kutoka.
    Na nzuri zaidi kuweka nia na kuhudhulia semina nayo ni hatua ya mafanikio kwani mambo huwa hayaji kwa kukudondokea mbele kama embe bila ya kuyatafuta wala kuyachuchumilia kwa hali zote.
    Niwapongeze wote walio hudhuhulia na waandaaji hii ni dhamila ya kusaidia na kufanya mambo ambayo wengi tunadhani sio rahisi kuyafanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X