Kuna usemi wa albert Einstein ambao binafsi huwa naupenda sana, unasema kwamba ujinga ni kufanya mambo yaleyale huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti. Hii ni kauli fupi ila yenye maana kubwa sana hasa kwetu sisi ambao tunataka kuufikia uhuru wa kifedha. Kabla hujawa na malengo ya kufikia uhuru wa kifedha, ulikukuwa umeridhika na ka kipato kako hata kama kalikuwa ni kadogo.
Ila sasa umeshakuwa na malengo ya kufikia uhuru wa kifedha. Na uhuru wa kifedha ni pale unapokuwa na fedha za kukutosha wewe kuishi maisha yako yote hata kama hufanyi kazi. Sasa lengo hili huwezi kulifikia kwa kuendelea kuwa na kipato chako hicho kidogo, unapaswa kuongeza kipato zaidi na zaidi ili kuhakikisha kuwa unalifikia lengo la kuwa na uhuru wa kifedha.
Na hii ndiyo sababu ya msingi kabisa ambayo inapaswa kukusukuma wewe kufikia malengo yako ya kifedha bila ya kurudi nyuma.
Makala hii Imeandikwa na godius Rweyongeza. Kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza basi endelea kutembelea mtandao huu. au Jiunge naye kwa kujaza taarifa zako hapa chini