Kama kuna faida ulizonazo. Zitumie vizuri


Shag alikuwa ni mmoja wachezaji wa kikapu ambao walifanya vizuri sana. Moja ya sifa ambayo anayo Shag ni urefu. Ana urefu wa mita 2.159. Kitu hiki kilimfanya kuwa mmoja wa wachezaji wachache wenye urefu kama wa kwake. Ambayo kwake ilikuwa ni faida.

Kwa upande wake Shag hii faida aliitumia vizuri sana kwenye kucheza na kuhakikisha kaba anacheza vizuri na kwa viwango vya hali ya juu sana.

Hakusema kwamba kwa kuwa mimi ni mrefu basi sitacheza sana kwa sababu nitafunga sana na hivyo nitakuwa nimeaonea wengine. Hakusema kwa kuwa wachezaji wengine ni wafupi kuliko mimi basi sitacheza.

Kitu kikubwa ni kwamba aliendelea kucheza zaidi  bila ya kuogopa.

Kitu hiki nataka kitufundishe kitu kimooja kikubwa sana, na kitu hik ni kwamba mara zote unapaswa kuwa unaangalia kile ulichonacho  na kukitumia vizuri kuliko kuanza kuangali kile ambacho hauna

Uwe na siku njema sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X