AKILI YA MKULIMA: mambo 12 ya kujifunza kutoka kwa mkulima unayopaswa kuyatumia kwenye maisha yako ya kila siku


Hata kama wewe siyo mkulima, hakikisha unasoma vizuri makala ya leo.

MARA KWA MARA UTASIKIA watu mbalimbali wakisema kwamba ,mimi nimezaliwa kwenye familia ya wakulima. Mimi ni mtoto wa mkulima. Ila wanavyokuwa wanaishi maisha yao inakuwa ni kinyume na masomo ambayo tunajifunza kwa wakulima. Kama wewe ni mtoto wa mkulima, ni wazi kuwa kuna mengi ambayo unaweza kujifunza kutoka kwenye familia ya kikulima ambayo unaweza kuyatumia kwenye maisha ya kila siku.

Kitu cha kwanza kabisa cha kujifunza kutoka kwa mkulima ni akili ya kutunza mbegu. Hakuna mkulima yeyote ambaye huwa anakula mbegu yote baada ya mavuno. Mkulima makini, baada ya mavuno, hata kama amepata mavuno ambayo hayatoshelezi, bado atatoa mbegu za kupanda mwakani. Anajua wazi kuwa akila mpaka mbegu, mwakani hatakuwa na kitu cha kupanda na kama hataweza kupanda basi maana yake kutakuwa hakuna mavuno.

Hii ni akili makini sana ambayo na wewe mwenyewe unapaswa kuwa nayo na unapaswa kuitumia kwenye maisha yako.

Inawezekana wewe siyo mkulima. Na inawezekana chanzo chako cha kipato hakitoki kwenye kilimo kama ilivyo kwa wakulima wengine, ila hii akili ya mkulima haupaswi kuiacha. Unapaswa kuambatana nayo popote pale utakapokuwa.

Kwa kila kiasi cha fedha ambacho utapokea mkononi mwako, kitu cha kwanza kabisa ambacho unapaswa kufanyia kazi ni kutoa mbegu. Fedha yoyote ile ambayo unatoa na kuweka akiba ni mbegu ambayo unaiandaa kwa ajill ya kuja kuipanda mwaka unaofuata.

Mkulima huwa anajua wazi kuwa mbegu hata kama ni kidogo, akiipanda mwisho wa siku atapata mavuno ambayo ni zaidi ya zile mbegu. Kama ameweka mbegu debe moja, akipanda hilo debe moja, hatapata tena tena debe moja. Badala yake atapata atapata magunia!

Na wewe linapokuja kwenye suala la fedha yako, haupaswi kula mbegu, badala yake unapaswa kupanda mbegu, ili uweze kula mavuno yanayotokana na mbegu.kwenye kitabu cha tajiri wa babeli kuna somo moja kubwa sana ambalo binafsi niliondoka nalo. Ni baada ya jamaa mmoja kwenye kitabu ambaye anafahamika kama Bansir kuomba ushauri kwa tajiri aliyekuja Babeli kutoka mji mwingine. Tajiri alimwambia kitu kimoja tu, kuwa kwa kila kipato ambacho unaingiza kwenye mfuko wako, kitu cha kwanza kabisa ambacho unapaswa kufanya ni kuweka akiba.

Bansir aliufuata huu ushauri, baaada ya mwaka mmoja alikuwa amepata kiasi cha kutosha kiasi kwamba litumia kiasi hicho kwenye kununua  punda. Tajiri alipokuja alimwambia kwamba, umekosea. Kitu cha kwanza kwako kufanya hakikupaswa kuwa kununua punda, maana kwa kufanya hivyo, maana yake unakuwa unakula mbegu za matunda yako. Wewe unachopaswa kufanya ni kutunza akiba yako na kuiwekeza ili uwekezaji huu uweze kukuletea mpaka wajukuu na vitukuu. Ni kutokea hapo sasa ndipo utakuwa unaruhusiwa kula wajukuu na vitukuu vyako. hii ni sawa na mkulima ambaye kwake

Mbegu ya kupandwa kwa mkulima huwa ni kipaumbele na tena huwa inatolewa ikiwa ya kwanza kabla ya matumizi mengine. Tena huwa inatolewa mbegu ambayo ni bora kabisa kuliko nyingine zote. Hakuna mkulima ambaye huwa anatunza mbegu iliyoharibika. Mbegu ambayo huwa inatunzwa ni ile ambayo ni bora kabisa. Hili pia litufundishe kuwa AKIBA, inapaswa kuwa ni kipaumbele cha kwanza. Siyo upate fedha na utumie yote mpaka iishe halafu ndiyo uje ukumbuke kuweka akiba, badala yake ni kwamba unapaswa kuweka akiba kwanza  halafu mambo mengine yatafuata baadaye.

uwe na siku njema.


One response to “AKILI YA MKULIMA: mambo 12 ya kujifunza kutoka kwa mkulima unayopaswa kuyatumia kwenye maisha yako ya kila siku”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X