Jinsi Ya Kufikia Ndoto Kubwa Hatua Kwa Hatua


Pata picha una ndoto ya kujenga hoteli kubwa ya kifahari…Yenye nyota saba. Mhh kama unaguna au kujiuliza kama hoteli ya aina hiyo ipo au haipo…
Ukweli mi kwamba ipo moja huko Uarabuni panaitwa Burj Al Arab iko Dubai.

Sasa kumbe moja tayari ipo, basi hiki ni kiashiria kingine kuwa na wewe unaweza kujenga hoteli yako ya aina ya hii….

By the way huu ni mfano, usije ukaacha kufanyia kazi ndoto eti kisa hapa nimeandika hoteli. Kuna kitu nataka nikwambie leo.. hivyo, kaa mkao wa kula.

Swali ni je unajengaje hoteli kubwa na kifahari hivyo?
Hela unaitoa wapi?
Nyenzo nyingine za kukuwezesha kujenga hoteli yako unazitoa wapi?

Hapa sasa ndipo nataka nikazie. Kuna vtu Vitano amnavyo unaweza kufanya ili kufanikisha ndoto yako hii.

KWANZA NI KUANZA KUIFANYIA KAZI MDOTO YAKO KWA UDOGO

Hapa ndipo watu wengi huwa wanashindwa kufanyia ndoto zao. Unakuta mtu ana ndoto kubwa ila haangalii ni kwa namna gani anaweza kuifanyia kazi kwa udogo. Ukweli ni kuwa mtu yeyote anatetaka kuhamisha mlima, sharti aanze kuhamisha mawe kidogokidogo.

Jiwe likitoka linakuwa limetoka. Halirudi. Hivyohivyo kwako mwenye ndoto kubwa. Kama una hii ndoto kubwa sana, anza kuifanyia kazi hata kama ni kwa udogo.

Kuthibitisha kuwa hili jambo ninalokwambia hapa, mimi mwenyewe nimekuwa nikilitumia kwenye uandishi wa vitabu. Watu wengi wanashangaa ni kwa namna gani nimeweza kuandika vitabu vingi kiasi hicho, ila ukweli mi kuwa sijaandika vitabu 20 vyote kwa wakati mmoja badala yake nikiandika vitabu hivi kidogokidogo, mwisho wa siku hiki kidogokidogo kimegeuka kuwa vitabu vikubwa na vingi.

Juzi mmoja wa watu ambao walisoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA alinitumia ujumbe. Alisema,

Nguvu ya Vitu Vidogo Soon Inanipa Nissan Dualis very Soon..

Hii nataka nikuoneshe kuwa ukiwa na lengo kubwa lolote, unaweza kukifanyia kazi hatua kwa hatua kwa kutumia NGUVU YA VITU VIDOGO ndiyo maana na wewe nakushauri usome kitabu hiki.

Kitabu hiki kinaenda kukupa Mwongozo wa hatua kwa hatua wa kifanyia kazi ndoto kuvwa sana. Kupata nakala ya kitabu hiki wasiliana na 0684408755 sasa ili utumiwe nakala hako. Nakala moja 20,000/-.

😊😊. Mara paap unaona bei, unaanza kujisema kitabu chenyewe bei kubwa😊😊. Sasa jamani ndoto yako si kubwa eti… Enewei tuachane na kitabu kwanza tuendelee..

PILI ni kuwa na juhudi kwenye kazi na shughuli zako zaidi. Yaani, ufanye kazi kwa juhudi na kukituma zaidi ya mtu yeyote yule. Mambo unayoyafanya kuelekea ndoto yako yawe mara kumi zaidi ya mtu wa kawaida

Kwenye kitabu chake cha THE 10X RULE; Mwandishi anasema kila kitu unachofanya kinapaswa kuwa na viwango vikubwa mara kumi zaidi ya wengine waliokuzunguka.

Uwe na ndoto kubwa zaidi ya mtu yeyote aliyekuzunguka (ndio maana tumeanza na mfano wa ndoto ya hoteli ya nyota saba)

Ufanye kazi kwa bidii na kwa juhudi mara 10 zaidi ya wengine. Na ukae na watu wanaofanya kazi kwa bidii na kujituma. Kama wewe unakaa kwenye chumba ambacho kuna watu wengine wanafanya kazi kwa bidii zaidi yako basi anza kupambana na kuanza kufanya kazi kwa bidii.

Tatu, weka akiba. Kwa kila kiasi unachopata usiache kuweka akiba kwa ajili ya ndoto na malengo yako. Akiba ni muhimu sana maana itakuja kukuinua na kukusaidia kufanikisha ndoto zako.

Hayo ni mambo matatu makubwa ambayo yatakusaidia wewe kufanikisha NDOTO ZAKO KUBWA.

Anza leo kuyafanyia kazi bila kurudi nyuma.
Kupata kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA wasiliana na 0684408755. Utatumiwa kitabu chako popote pale ulipo.

Makala hii imeqndikwa na GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
www.songambele.co.tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X