Mara moja siyo mbaya


Mara kwa mara utasikia watu wanasema mara moja siyo mbaya. Yaani, kwamba kufanya jambo mara moja halafu ukaacha siyo kitu kibaya.

Kwenye ulimwengu wa mafanikio, mara moja ni mbaya sana.

Unahitaji ufanye vitu kwa mwendelezo na mara kwa mara, bila kuacha kwa kuda mrefu ili upate matokeo.

Kama ni akiba unapaswa kuweka akiba kila siku hata kama ni kidogo, ufanye hivyo kwa mwendelezo bila kuacha. Baada ya muda vitu vidogo utakavyokuwa unafanya vitakuletea matokeo.

Kama ni kujitlfunza. Fanya hivyo kila siku bila kuacha.

Kama ni kuamka asubuhi na mapema, fanya hivyo kila siku.

Ukifanya mara moja ni mbaya sana. Nakubaliana na Bruce Lee aliyesema kuwa
“Sina hofu na yule aliyejaribu mishale elfu moja mara moja, lakini nina hofu na yule aliyejaribu mshale mmoja mara elfu kumi.”

Akiwa anaamaanisha kwamba kufanya mara mwendelezo Kuna nguvu kubwa sana kuliko kufanya kwa kustukiza mara moja.

Hatua ya kuchukua leo.

  1. Chagua kitu kimoja cha kufanyia kazi (kuweka akiba, kuwekeza, kujifunza n.k)
  2. Kifanye hicho kitu kwa mwendelezo kila siku bila kuacha.
  3. Pima matokeo yake baada ya siku 100.

Kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X