TAARIFA mbili Muhimu kuhusu semina ya KUONGEZA KIPATO MARA MBILI


Rafiki yangu mpendwa, salaam. Hongera kwa kazi. Leo nina taarifa mbili muhimu sana kuhusu semina ya KUONGEZA KIPATO CHAKO MARA 2.

Taarifa ya kwanza ni kuhusu watu ambao hawatalipia semina hii. Ndio, kuna ambao hawatalipia semina hii, watahudhuria bure. Na taaarifa ya pili ni vigezo vya kushiriki.

Maana wengi walikuwa wanafikiri kila mmoja anaweza kushiriki, ila ukweli ni kuwa sipokei kila mtu kwenye hii semina. Kuna vigezo unapaswa kuwa navyo. Kama hauna hivi vigezo semina imekupita. Nataka baada ya semina hii niweke nguvu kwa wale wachache watakaoshiriki, niwafuatilie kwa ukaribu kwa mwaka mmoja ujao mpaka kila mtu apate matokeo. Na ufuatiliaji wa aina hii unahitaji muda na watu ambao wako siriazi. Hivyo, wewe unaweza usikidhi vigezo….fuatilia kwa umakini makala hii ili ujue kama umo au haumo.

TAARIFA YA KWANZA:

Wote walioshiriki Semina ya ana Kwa ana Morogoro hawalipii Semina ya kuongeza Kipato mara mbili.

Kama ulishiriki Semina ya ana Kwa ana iliyofanyika MOROGORO mjini tarehe 24 Juni, hutalipia semina hii ya mwezi wa Tisa. Unachotakiwa kufanya sasa ni kuendelea kujiandaa na kujipanga kwa ajili ya kuja kupata mafunzo haya ya kipekee ya Semina.

Andaa kalamu Kwa ajili ya kuchukua notes.
Andaa notebook.

Lakini pia rudia mambo tuliyokubaliana kwenye semina ya Morogoro. Kama hujaanza kuyafanyia kazi, hakikisha unaanza kuyafanyia kazi. Nakuhakikishia kuwa hutaweza kupata matokeo, endapo hutachukua hatua. Nataka mwakani tunapokuna uwe umepiga hatua. Kama hili ni gumu kwako, basi basi yajayo yanaweza kuw magumu zaidi kwako.

Pangilia ratiba yako kiasi kwamba Kila siku utapata muda Kati ya dakika 45-60 za kufuatilia somo la siku husika na kushiriki kwenye mjadala.

Kumbuka, Semina hii itafanyika tarehe 24-30 Septemba.

Itafanyika kwenye kundi letu special la whatsap.

Utaratibu wa SEMINA utakuwa hivi.

Asubuhi na mapema sana (saa 11 alfajiri) Tutakuwa tunapata SoMo la siku husika. SoMo Hilo litatolewa Kwa mfumo WA sauti na maandishi pia.

Hivyo, utakuwa na uchaguzi wa au kusoma SoMo la siku la siku hiyo au Kusikiliza.

Baada ya kusoma SoMo la siku hiyo utakuwa na nafasi ya kuuliza maswali au kutoa maoni Yako.

Baadaye jioni, Tutakuwa tunakuwa na mjadala wa pamoja. Mjadala wa pamoja utakuwa ni saa 1-2 jioni Kila siku Kwa siku zote saba za Semina.

Mada zitakazofundishwa Kwenye hii Semina ni

 1. Kwa nini unahitaji kuongeza kipato chako mara 2
 2. Hatua sita Muhimu za kufuata ili uongeze kipato chako mara 2 ndani ya mwaka mmoja
  3.Jinsi ya kuweka yatakayokupelekea kuongeza kipato chako mara 2
 3. Vyanzo muhimu vitakavyokuwezesha kuongeza kipato chako mara mbili NDANI YA MWAKA MMOJA
 4. Kanuni ya 80/20 kwenye kuongeza kipato chako.

5.Namna ya kutengeneza mshahara nje ya mshahara

 1. Kwa nini unahitaji kutengeneza mshahara wako mwenyewe (nje ya mshahara ya mshahara wa kawaida)
 2. Uwekezaji. Msingi mkuu wa kutengeneza mshahara nje ya mshahara.
 3. BIASHARA: nyenzo muhimu ya kuongeza kipato chako mara mbili zaidi ndani ya mwaka mmoja
 4. Kuanzisha biashara yako – wazo na mkakati
 5. Usimamizi wa biashara na ukuaji wa kipato
 6. Mbinu za kujiongezea mauzo na mapato
 7. Kutambua fursa za kukua na kupanua biashara yako
 8. Kupima mafanikio na kutengeneza mkakati wa baadaye
 9. mtandao wako ndiyo utajiri wako: na jinsi ya kujenga mtandao utakaokupa fedha
 10. Biashara ni mahusiano na namna ya kuyajenga

17: ELIMU YA KIFEDHA: KUDHIBITI NA KUKUZA FEDHA ZAKO

 1. UTAJIRI: misingi mikuu ya kujenga utajiri isiyoyumba
 2. Jinsi ya kuandaa utajiri utakaorishwa mpaka kwa watoto na wajukuu zako
 3. Hitimisho

Haya ndiyo mambo ya msingi Sana tutakayoona kwenye hii Semina. Kiufupi hii Semina so watu ambao wanataka kuremba mwandiko.

TAARIFA YA PILI

Hii Semina ya watu ambao wanataka kuchukua HATUA. Semina ya watu ambao wanataka kufanya Vitu vya tofauti.

Watu ambao wanataka kupata MATOKEO makubwa.

Watu ambao wakielekezwa wanafanya KAZI. SIYO unajifunza kitu hapa, halafu unaenda kufanya kingine halafu unaendelea kulalamika.

Hii Semina SIYO SEMINA ya watu wanaolalamika, wazembe na ambao hawataki kufanya KAZI.

Watu wanaojua kuwa kazi yangu ni kuwaongoza, kuwakochi (coaching) na kuwasukma kwenye hatua ya ziada. Na wapo tayari kusukumwa ili wafikie hizi hatua za ziada.

Watu wenye mtazamo chanya, ambao wapo tayari kupokea mrejesho kama ulivyo bila kurembwa.

Watu ambao hawana visingizio. Ambao wapo tayari kufanyia jazi tutakachojifunza mpaka wafikie malengo na ndoto zao.

Kama huna hizo sifa, tafadhali usilipie kuhudhuria hii Semina. Bora tu Hela yako uiweke sehemu nyingine ambapo utakuwa unaiona. Na nikigundua umelipia ila huna hizo sifa, nitakurudishia hela yako.

Kitu kikubwa cha kufahamu ni kuwa hatutaishia tu kupata Semina. Bali ufuatiliaji wa karibu wa Kila Mmoja. Mpaka Mwezi wa SITA mwakani. Hivyo, kama wewe hutaki kufuatiliwa kwa ukaribu Kwa kipimdi Hiki chote mpaka mwakani, usilipie hii Semina…..

Ada ya Semina ni 20,000/- tu.

Namba ya malipo 0684408755.

Mara baada ya Semina kama utakuwa hujaridhishwa na mafunzo, tutakurudishia Hela yako.

Kama wewe una sifa za kuhudhuria. Basi kinachofuata ni wewe kulipia. Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

Karibu Sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X