Kuanzia Tarehe 1 Agosti mpaka tarehe 8 tumepata nafasi ya kushiriki kwenye maonesho ya nanenane. Hii ni mara yetu ya pili kushiriki kwenye haya maonesho makubwa tukiendelea kutoa elimu na kuwahahamasisha watu kujifunza na kusoma vitabu.
Mwaka huu kama kawaida, tumepata washiriki wengi, ambao wametembelea banda letu. Umekuwa ni mwaka mwingine bora sana.
Kutokana na majukumu kuwa mengi mwaka huu, nilishiriki baadhi ya siku tu. Na siku nyingine nilikuwepo kwa baadhi ya masaa, ila kwa kila niliyepata nafasi ya kuongea naye, nilimsisitiza jambo moja kubwa sana. Na jambo hili
Ni kuwa na akili ya mkulima.
Kwa kuwa yalikuwa ni maonesho ya wakulima. Nilitoa mfano wa mkulima kwa kila mtu aliyeshiriki maonesho. Unajua akili ya mkulima ikoje?
Akili ya mkulima ni kwamba, anapovuna shambani. Hata kama mavuno ni kidogo kitu cha kwanza anachofanya ni kutoa mbegu atakayopanda mwakani. Mkulima ni sharti afanye hivi bila kujali mavuno aliyopata ni kidogo. Na mkulima anayefanya hivi tunaweza kumwita mkulima mwelevu.
Aidha, mkulima ambaye anakula au anauza mazao yote baada ya kuvuna, bila kubakiza mbegu tunaweza kumwita mkulima mpumbavu. Hafikirii kesho na hana maono yoyote ya kesho. Wewe unapaswa kuwa kama mkulima mwerevu hasa linapokuja suala zima la fedha unazopokea.
Kipato chako unachopata hata kama ni kidogo, unapaswa kutoa kiasi kidogo na kukiweka kama akiba, akiba hii itakusaidia wewe baadaye. Usile kila kitu ukajisahau.
Usitumie kipato chako chote. Mara zote akiba yako, ipe kipaumbele. Weka kiba kama mbegu mbayo unakuwa umeitunza kwa ajili ya kesho yako.
Baada ya kumaliza kusema hayo, nilimwasa kila mtu apate nakala ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA pamoja na NGUVU YA VITU VIDOGO ili aende kuanza kujijengea utaratibu wa kuweka akiba.
Sasa basi, nikusihi kitu kimoja tu rafiki yangu. Inawezekana hukushiriki maonesho ya nanenane, ili kupata wosia kama huo. Ila kitu kimoja cha uhakika ni kwamba, unahitaji kuwa akili ya mkulima!
Unachotakiwa kufanya sasa ni kitu kimoja tu.
Kupata vitabu viwili ambavyo kila mshiriki wa maonesho haya amepata. Kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA, pamoja na kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.
Hivi ni vitabu viwili vizuri sana ambavyo unapaswa kuwa navyo. Watu wengi waliosoma vitabu hivi wamevipenda sana na mwisho wa siku wameanza kuchukua hatua za tofauti. Natamani na wewe uwe miongoni mwao!
Kupata vitabu hivi ni rahisi sana, tuwasiliane kwa 0684408755 au 0755848391
Kabla sijasahau Ningependa nikutaarifu kuwa tutakuwa n semina kubwa ya mtandaoni. Semina hii inaenda kufanyika tarehe 24-30 septemba. Itakuwa ni semina babu kubwa ambapo tunaenda kuona JINSI YA KUONGEZA KIPATO CHAKO MARA 2 NDANI YA MWAKA MMOJA.
Zifuatazo ni mada ambazo tutaongelea kwa undani.
SIKU YA KWANZA:
KARIBU KWENYE SEMINA YA KUONGEZA KIPATO MARA 2
Katika hii siku tutaona
Kwa nini unahitaji kuongeza kipato chako mara 2
Hatua sita Muhimu za kufuata ili uongeze kipato chako mara 2 ndani ya mwaka mmoja
Jinsi ya kuweka yatakayokupelekea kuongeza kipato chako mara 2
SIKU YA 2
Vyanzo muhimu vitakavyokuwezesha kuongeza kipato chako mara mbili NDANI YA MWAKA MMOJA
Jinsi ya kutumia kanuni ya 20/80 kwenye kujenga kipato chako mara 2 ndani ya mwaka mmoja.
Siku ya tatu: JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA
Ndani ya hii siku tutazama ndani zaidi na kuona….
Kwa nini unahitaji kutengeneza mshahara wako mwenyewe (nje ya mshahara ya mshahara wa kawaida)
Namna ya kutengeneza mshahara nje ya mshahara
Uwekezaji. Msingi mkuu wa kutengeneza mshahara nje ya mshahara.
Ukweli ni kwamba, mpaka hapo ada yako ya semina itakuwa imeisha, ila semina itakuwa inaendelea😊😊
SIKU YA NNE: BIASHARA: NYENZO MUHIMU YA KUONGEZA KIPATO CHAKO MARA MBILI ZAIDI NDANI YA MWAKA MMOJA
Kuanzisha biashara yako – wazo na mkakati
Usimamizi wa biashara na ukuaji wa kipato
Mbinu za kujiongezea mauzo na mapato
Kutambua fursa za kukua na kupanua biashara yako
Kupima mafanikio na kutengeneza mkakati wa baadaye
SIKU YA TANO: MTANDAO WAKO NDIYO UTAJIRI WAKO:
Jinsi ya kujenga mtandao utakaokupa fedha
Mbinu za kuwafikia wateja au watu watakaokuwa tayari kutoa fedha mfukoni kukulipa au kununua bidhaa zako
Biashara ni mahusiano na namna ya kuyajenga
Siku ya SITA: ELIMU YA KIFEDHA: KUDHIBITI NA KUKUZA FEDHA ZAKO
Uelewa wa msingi wa fedha na bajeti
Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima
Kuweka akiba na kuwekeza kwa ufanisi
Kudhibiti madeni na mikopo
SIKU YA SABA: UTAJIRI: MISINGI MIKUU YA KUJENGA UTAJIRI ISIYOYUMBA
Jinsi ya kuandaa utajiri utakaorithishwa mpaka kwa watoto na wajukuu zako
SIKU YA NANE: HITIMISHO
Muundo wa uendeshaji wa semina.
Masomo yatatolewa kupitia kundi maalumu la Whatsapp. Yatatolewa kwa njia ya maandishi na sauti pia. Hivyo, kama utakuwa umebanwa na huwezi kusoma, utakuwa unapata nafasi ya kupata somo la siku hiyohiyo kwa mfumo wa sauti.
Tutakuwa na kundi special la whatsap. Kwenye kundi hili utaungwa tu punde baada ya kulipia walau nusu ya gharama ya semina
Gharama ya semina ni 20,000/- tu. Na inalipwa kupitia 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
Kwa kipindi chote cha semina, masomo yatakuwa yanatolewa mapema kabla ya saa 11 alfajiri. Utapata muda mzuri wa kusoma au Kusikiliza somo la siku husika. Baada ya kusoma somo hilo, utaruhusiwa kuuliza maswali.
Jioni saa 1-2 tutakuwa tunakuwa na mjadala wa pamoja.
Hii itakuwa ni kwa siku zote saba za semina.
Kiukweli. Naam, kiukweli, itakuwa na semina bora sana kuwahi kutokea!
Rafiki yangu, hii semina haupaswi kuikosa hata kidogo. Thibitisha ushiriki wako kwenye semina hii sasa. Lipia kwa 0684408755. Kama una maswali uliza kwa kupiga 0684408755 au 0755848391