Ujiajiri Au Uajiriwe? Ukweli Mchungu….


Suala la kuajiriwa na kujiajiri limekuwa linapata mjadala mkubwa sehemu mbalimbali. Kwenye vyombo Vya habari, Kwa wahamasishaji, wanasiasa, viongozi wa Serikali ma dini pia.

Hata hivyo wengi ambao Huwa wanahamasisha kujiajiri, wenyewe hawajawahi kujiajiri😊😊.

Hiki kitu a uta wa siutata Kwa wale wanaofanya KAZI huu ushauri. Yaani, wanaufanyia KAZI, lakini wanaokwama wanakuwa hawana mtu sahihi wa kuwashika mkono.

Kwenye makala ya Leo tunaenda kuona mbichi na mbuvuvkuhusu kujiajiri na kuajiriwa na mwisho wa siku tutaina ni hatua Gani unaweza kuchukua. Makala ya leo ni jibu kwa swali ambalo aliniuliza rafiki yangu mmoja. kabla hatujaebdelea zaidi tuone swali lake.

Habari yangu ni njema kabisa ESTA.

  1. Kwanza nikupongeze Kwa ujasiri huu WA kujifanyia tathmini na kuona NGUVU na kile ulichonacho na unachoweza kufanya.
  2. Pili ni ukweli Kuwa tumekuwa tunahamasisha watu kujiajiri, ila ukweli mwingine ni kuwa siyo rahisi SANA. kujiajiri Kuna mengi. Hakuna uhakika WA kipato. Kuna wakati unaweza kupitisha Muda hujapata kipato na Kuna wakati unaweza kupata Hela nyingi ndani ya Muda mchache kuzidi hata mishahara kadhaa ya mwajiriwa. Yote hayo yapo, ila ukweli Bado unabaki Kuwa kujiajiri siyo rahisi
  3. Kwa upande wako, nakushauri utafute KAZI kwanza. Kujiajiri kunaweza Kuwa rahisi ukiwa na chanzo kingine Cha kipato ambacho ni Ajira. Lakini pia kujiajiri kunaweza Kuwa kugumu ukiwa na Ajira. Ugumu wake unakuwa hivi, kwanza unakuwa na uhakika WA kipato Kila mwezi. AKILI yako inalemaa na inakuwa haitaki kujihangaisha Zaidi na Zaidi. Hivyo, utegemezi wako wote unauweka kwenye mshahara.

Lakini pia KUANZISHA BIASHARA ukiwa umeajiriwa maana yake ni kwamba unapaswa kugawa Muda wako vizuri. Kati ya muda wako na muda WA mwajiri. Na unapaswa kujituma haswa Ili utimize majukumu yako na ya mwajiri. Unapaswa kuwa SIKU mbili ndani ya simu Moja, SIKU ya kazi za mwajiri na siku ya BIASHARA yako na hatimaye muda na familia. Siyo rahisi.

  1. Lakini sambamba na hayo yote Bado nakushauri ESTA katafute KAZI kwanza uajiriwe. Ukishapata KAZI sasa ndiyo tutapanga mpango mzuri WA KUANZISHA BIASHARA. Hii Kwa upande wako itakuwa na faida ya kupata mtaji ambao itakusaidia KUANZISHA BIASHARA. Tafadhali naomba ufahamu kuwa unavyoajiriwa, ajiriwa ukiwa na PLAN B kichwani. Plan ya SIKU Moja kutengeneza Kitu cha kwako.

Sasa swali kinakuja unapataje Ajira?

Binafsi sijawahi kuomba KAZI. Sijawahi kutuma CV sehemu yotote Ile. Ila kama ningekuwa naomba KAZI Leo hii. Ningefanya yafuatayo.

Kwanza, ningeandaa vyeti vyangu vyote va msingi.
Pili, ningechagua kampuni ambazo nataka kufanya nazo KAZI. Ningetafuta hata kampuni 50 za kuanza nazo.

Tatu, ningetuma maombi yangu kwa wanaohusika kuajiri kwenye hizi kampuni nilizochagua, ningeendelea kuwafuatilia Kwa ukaribu hata Kwa kuwapigia simu Ili nijue kama wana mpango wao.

VITU vingine viwili vya ziada ambavyo ningefanya vingekuwa ni
Kujiunga na mtandao WA LINKELDN. Huu ni mtandao WA watalaam. Waajiri wengi wako huku. Huu mtandao siyo kama Instagram ambapo Kila MTU anajiunga. Wanaojiunga huku ni watu makini sana. Huku Sasa ningefuatilia fursa za ajira zilipo. Lakini pia ningeanza kujenga ukaribu na watu ambao ningependa kufanya KAZI kwenye taasisi zao. Na hata kuwauliza kama Wana nafasi au wanafahamu sehemu yenye nafasi ambapo naweza kuajiriwa.

Sambamba na Hilo ningetembelea ofisi mbalimbali ambazo ninataka kufanya nazo KAZI. Hapa ningezitembelea ana Kwa ana na kuomba kuonana na bosi wao. Kitendo Cha kuonana na bosi TU, kingenifanya nimweleze Mimi ni nani na ninaweza Nini. Ningemweleza ni Kwa namna Gani nitakuwa MTU WA msaada kwake.

Hiki kipengele ndiyo kugumu kuliko Vyote ambavyo nimetaja hapo juu. Wengi wanakiogopa hiki, ila kama ningekuwa Mimi ninayetafuta KAZI. Hiki ndiyo ningekipa kipaumbele Zaidi.

Changamoto inakuja kwenye kuonana na bosi hasa unapoenda kwenye kampuni husika. Wasaidizi WA mabosi Huwa wanakuwa wagumu sana kukukutanisha na mabosi zao.
Wanataka wajue Nini hasa unachofuata Kwa bosi na ukiwaambia wanakukatisha tamaa na kukwambia Hilo haliwezekani. Ila kumbe kama ungekutana na bosi ingekuwa ni rahisi sana kwako kumwambia unachotaka akakubali.

Sasa basi, ambacho ningefanya. Kiuhalisia hiki ndicho Huwa nafanya. Mbali na kuwa sijawahi kuomba KAZI kama nilivyokwambia, ila Huwa ninaonana na wakurugenzi wa kampuni mbalimbali Kwa ajili ya shughuli zangu. Wiki hii TU nimeshatembelea kampuni na taasisi 14 na Leo nitaendelea kutembelea kampuni na taasisi zaidi. Kati ya hizo kampuni na taasisi 14. Ni kampuni 4 tu ambazo nimeona na bosi Moja Kwa Moja. Nyingine Kumi nimeishia Kwa wasaidizi ambao wameniblock nisionane na bosi wao na kampuni nyingine bosi alikuwa amesafiri au hayupo ofisini Kwa wakati huo.

Kati ya hao wanne, ni mmoja tu ambaye tumekubaliana Kitu cha maana na Leo saa SITA mchana ninaenda kuongea na wafanyakazi wa taasisi yake kuwafundiaha Kuhusu UMUHIMU WA KUSOMA VITABU na Kuweka AKIBA.

Mwingine ameniambia niende mwisho wa mwezi.

Nataka kusema njni, ninachotaka kukuonesha hapa ni kwamba hiki Kitu siyo rahisi ila kinawezekana.

Naomba nimalizie Kwa kusema kwamba chagua mpango wako ambao utaufanyia KAZI. Ufanyie KAZI Kwa uhakika bila kuacha. Nina hakika hili utalifanikisha.

Unafanyaje Sasa baada ya kupata KAZI?
Wengi Huwa wanajisahau sana bada ga kupata Ajira. MTU anapta Ajira anasahau kuwa ana ndoto na malengo ya kujiajiri. MTU anasahau Kuweka akiba. MTU anasahau kuwekeza.

Hiki ni kitu kibaya, kwani Kwa muda unapokuwa na Ajira utaona kuwa maisha umeyapatia, maana hata ukiutumia mshahara mwisho wa mwezi mshahara mwingine utakuwepo tu. Ila ambacho Haupaswi kusahau ni kuwa unapaswa KUAJIRIWA na PLAN B Kichwani. Plan ya kutengeneza kipato kingine nje ya Ajira.

Ndiyo maana unapaswa kuweka akiba, kuwekeza n.k.

Kwa Leo nadhani inatosha.
Mwisho kabisa uliniomba vitabu vizuri kutoka kwangu Vya kusoma. Naomba usome vitabu hivi Kwa mpangilio wake kama ninavyovitaja hapa JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA na JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO.

Lakini pia mwezi wa Tisa tutakuwa na SEMINA ya mtandaoni (online). Hii ni SEMINA ya KUONGEZA KIPATO CHAKO mara mbili ndani ya mwaka mmoja. Kwenye hii semina moja ya mada tutakazoongelea ni JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA. Tutaongelea vitu vingine Vingi ambavyo vitakufaa wewe kama mpambanaji Makini. Hivyo, nashauri usiache kuhudhuria semina hii ya mtandaoni ambayo itaanza tarehe 24 na kumalizika tarehe 30.

Semina itafanyika Kwenye kundi maalumu la whatsap na gharama ya SEMINA itakuwa ni 20,000/-
Tafadhali hakikisha unahudhuria semina hii. Unaweza kuwasiliana na msaidizi wangu 0684408755 na Kuweka mpango wako WA kulipia. Unaweza kulipia hata buku au jero. Unaweza kulipia Kila siku kiasi kidogo, unaweza kulipia Kila wiki kiasi Fulani au Kila mwezi. Unaweza pia kulipia mara moja.

Nimekupa taarifa mapema Ili usije kukosa mambo mazuri.

Asante sana

Karibu sana na Kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X