Cha kufanya kama unaanzia chini kweye maisha


Rafiki mpendwa salaam, bila shaka unaendele vizuri kabisa. Hongera kwa kazi. Mimi naendelea vizuri nikiwa hapa Morogoro mji kasoro bahari.

Siku ya leo nataka nikwambie kitu kimoja ambacho unapaswa kufanya kama unaanzia chini kwenye maisha. Unajua ni kitu gani hiki.

Kwanza ni kuchagua kitu ambacho utafanya. Hiki ni muhimu sana, watu wengi huwa hawapati nafasi ya kufanya kitu kama hiki. Huwa wanajikuta kwamba wanafanya kila kitu kwenye maisha yao. Wewe haupaswi kuwa mtu wa aina hiyo. Chagua kitu kimoja ambacho utaamua kukifanya kwa viwango tena vya juu  sana bila kujali nini kinatokea kwenywe maisha yako.

Baada ya kuchagua hikl kitu kimoja, weka nguvu zako zote kwenye hiki kitu.

Jifunze kuhusu hiki kitu. Ni kweli unaweza kufanya mambo mengi, lakini jipe nafasi ya kukua na kufanya jambo moja kwa undani na kwa uwezo wa hali ya juu sana. Kwa hiyo, usihangaike na kila kitu.

Hili jambo ninalokwambia hapa unaweza kulichukulia poa sana. Lakini jambo hilihili ndilo litakalokuwezesha kulipwa zaidi kwa hapo baadaye. Maana kama utachagua jambo moja, na jambo hili ukaamua kujifunza na kuliewa kwa undani na kuhakikisha kwamba umelielewa kuliko mtu mwingine yoyote. Lakini pia ukaenda mbali zaidi na kuhakikisha kwamba hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kulifanya zaidi ya wewe maana yake utaweza kulipwa zaidi ya mtu mwingine yeoyote Yule ambaye amekuzunguka kwenye jamii yako.

kinachoponza wengi ni kwamba huwa wanahangaika na mamb mengi kwenye maisha yao, kiasi kwamba huwa wanashindwa kufanikisha jambo moja kwa viwango vikubwa sana. Wewe haupaswi kuwa mtu wa aina hiyo, badala yake unapaswa kuwa mtu ambaye unaweka nguvu zako kwenye jambo moja na unahakikisha kwamba hilo jambo llinafanikiwa kwa viwango vikubwa sana.

Kitu kingine cha muhimu ambacho unapaswa kufahamu ni kuwa ili uweze kufanikisha jambo la aina hii unapaswa kuhakikisha kwamba unafanya jambo ambalo umechagua kila siku bila kuacha. Kama siyo kila siku basi ufanye hilo jambo mara kwa mara

Kwa mfano kama umechagua kuandika makala kama hizi unapaswa kuwa unafanya hivyo kila siku bila ya kujali n ikitu gani amabcho kinatokea kwenye maisha yako. Kitu hiki kitakuwezesha kujenga nidhamu kwenye uandishi lakini pia kitakupa nidhamu ya kuwa unajifunza kila siku ili uweze kupata kitu cha kuandika. Maana huwezi tu kulala na kuamka na kuandika bila ya maandalizi.

Lakini pia kitu kama hiki kitakufanya ubobee kwenye uandishi kuliko mtu mwingine yeyote ambaye amekuzunguka. Kwa hiyo anza kulifanyia kazi hilo.

Kama umechagua kuweka akiba, inaweza kuwa kila siku kama kipato chako kinaingia kila siku. Lakini kama kipato chako kinaingia kila wiki, basi unaweza weka akiba kila wiiki bila ya kucha.

Na endapo kipato chako kinaingia kila mwezi basi unaweza kuweka akiba kila mwezi bila ya kcuaha. Kitu hiki kitakufanya urudie kufanya kitu kile kile kila mara na mwisho wa siku utajikuta kwamba umebobea na kufanya jambo hilo liwe tabia yako.

Kama umechagua kuwekeza, mfano kwenye soko la hisa, unaweza kuwa unawekeza kila wiki, au kila mwezi. Kuwekeza kwenye soko la hisa ni vigumu kufanya hivyo kila siku, lakini unaweza kufanya hivyo kila siku za wiki, yaani jumatatu mpaka ijumaa, maana soko la hisa huwa halifunguliwi jumamosi na jumapili.

Lakini kama unanunua vipande kwenye mifuko ya vipande kama utt na faida fund ya whi basi unaweza kuwa unanunua kila siku, bila ya kuacha.

Kama ni mazoezi unaweza kufanya kila siku kwa dakika kadhaa.

Ni muhimu sana kurudia kufanya jambo na kulifanya kila mara bila ya kuacha.

Hiki kitu kitakufanya uweze kubobea kwenye hilo jambo na uweze kulifanya kwa weredi wa halil ya juu sana.

Kwa hiyo kama unaanzia chini kumbuka kufanya yafutayo.

Kwanza kuchagua jambo moja la kufanya

Pili lifanye jambo hilo kila mara au kila siku na kwa kurudia rudia bila kuacha na kwa nidhamu kali sana

Mwisho wa siku vitu hivi vidogovidogo unavyofanya utakuta kwamba vimekua na kuwa vikubwa. Ni jukumu lako sasa kuhakikisha kwamba umefanya hivyo.

Mwanzoni matokeo yanaweza yasionekane, lakini kadiri unavyoendelea kufanya bila ya kucha kwa muda mrefu utajikuta kwamba umeweza kufanya jambo hilo kwa viwango vikubwa sana.

Unapokuwa unaanzia chini, unakuwa hauna kitu. Ni nidhamu yako ndiyo itakayokuweka kwenye ramani, bila ya nidhamu utaishia kubaki hukohuko ulipo chini.

Ndiyo maana tangu mwanzoni nimekwambia kwamba kama unachagua kufanya jambo unapaswa kulifanya kwa kulirudia rudia mara kwa mara, bila ya kuchooka na bila yakurudi njyuma. Nadhani hapo umenielewa vizuri sana rafiki yangu.

KAMA MAMBO NI RAHISI HIVI KWA NINI WATUWENGI HUWA HAWAFANYI.

Vitu vya kujirudiarudia huwa havipendwi sana na watu. Watu huwa wanapenda vitu vipya. Na akili zetu ziko  hivyo, zinapenda kuona kitu kipya kila mara, hivyo vinapofanya kitu mara ya kwanza na mara ya pili zinaanza kuzoea kitu hicho. Na mwisho wa siku kitu hichocho kinaanza kuchukuliwa poa.

Kwa mfano, mtu anaanza kuweka akiba mwanzoni. Lakini anakosa uendelevu, kumbe ule mwendelezo wa kile kitu ndiyo utakaokusabibishia wewe uweze kufiikia mafanakio makubwa na siyo kufanya mambo mengi ya tofautitofauti kwa nyakati tofauti tofauti. Hivyo, kazi yako kubwa na jukumu lako kubwa ni kuhakikisha kwamba ukishajua vitu sahihi vya kufanya, basi vitu hivyo unavifanya kwa msimamo bila ya kuacha kwa muda mrefu.

Kwa mfano leo umejua kwamba ni muhimus ana kwako kuweka akiba akiba. Hili jambo usilifanye tu kwa siku moja kwa sababu unataka ulifanye kwa siku hiyo, badala yake lifanye kwa mwendezo na siku nyingi zinazo bila ya kuacha. Ni mwendelezo tu ndiyo utakaokupa matokeo. Kumbe badala ya kufanya hilo jambo na kuacha na kutafuta jingine. Lifanye hilohillo moja kwa mwenzelezo na kwa muda mrefu bila ya kuacha. Hiki kitu kitakupa matokeo makubwa sana rafiki yangu ambayo hata hapo mwanzoni wewe mwenyewe ulikuwa hutarajiii.

Ningependa kusikia kutoka kwako siku ya leo ni kitu gani aambacho umechagua kufanya kwa msimamo na kwa muda mrefu bila ya kuacha.

Naksuahauri, zaidi usome kitabu cha NGUVU YAKUCHUKUA HATUA YA KWANZA: Na Kwa Nini Unapaswa Kumaliza Kile Ulichoanza. KWENYE HIKI kitabu nimeelza kwa undani kwa namna gani uanapaswa kuanza kufanyia kazi vitu ambavyo unapenda kufanyia kazi bila ya kucha , lakini pia niemeelza kwa undani ni kwa namna gani unapaswa kuendeleza kile ambacho tayari umeanza kukifanyia kazi.

Kitabu hiki unaweza kukipata mtandao ni hapa

Hardcopy ni 25,000 unaweza kuipata kwa kulipia 25,000/-. Lipia kwenda namba ya simu 0684408755. Ukishalipia tuma taarifa zako ili utumiwe kitabu popote pale ulipo. NB: Gharama za kusafirisha ni juu yako.

Ukishalipia utanitumia jina lako ili niweze kukutumia kitabu jhiki.

Kila la kheri

Makala hii imeandikwa nami rafiki yako wa ukweli

GODIUS RWEYONGEZA, unaweza kuwasiliana nami kwa namba ya simu ambayo ni 0755848391

barua pepe ni godiusrweyongeza1@gmail.com

Kupata vitabu vyangu vyote wasiliana na 0684408755 sasa au BONYEZA HAPA kuvipata kwa njia ya mtandao.

Asante sana na karibu sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X