Rafiki yangu mpendwa, salaam
Bila shaka unaendelea vizuri kabbisa. Hongera kabisa kwa siku hii nyingine ya kipekee. Leo ni Jumamosi ya tarehe 16, mwezi wa tisa mwaka 2023. Ni siku bora kabisa ambayo naamini umeweza kuitimia kwa viwango vikubwa.
Siku ya leo kuna kitu kimoja tu ambacho ningependa kukwambia na kitu hiki siyo kingine bali ni kitu ambacho unapaswa kuwa na wasiwasi nacho. Najua sana kwenye maisha yako kwamba unakuwa na wasiwasi na vitu vingi sana kwenya maisha yako. Unaweza kuwa ni wasiwasi kwamba ukianzisha biashara inaweza kufa. Au wasiwasi kwamba ukiongea na mtu fulani kuhusiana na jambo lako anaweza kukukatalia.
Imethibitishwa mara kwa mara kwamba vitu vingia ambavyo watu huwa wanaogopa, huwa havitokei kwenye uhalisia. Karibia asilimia 90 na zaidi uya vitu unavyoogopa havitakuja kutokea na vingine unavyoogopa havipo kabisa.
Hivyo, linapokuja suuala zima la kuogopa linakuwa halina maana. Kitu pekee unachopaswa kuogopa ni kile ambacho kinakuwekea wewe ukomo wa kutumia uwezo wako.
Kulinganisha na vile tunavyopoapswa kuwa, alisema Dr. James Wiliiam, watu bado wameamka nusu.
Hii ndiyo kusema mimi na wewe tuna uwezo mkubwa sana ambao hata hatuutumii. Unapaswa kuanza kujisukuma mara moja kuutumia uwezo wako uliolala ndani yako.
Kama watu waliofanya makubwa mpaka sasa hivi wametumia asilimia chini ya kumi. Watu kama akina Steve Jobs ambao wamegudua vifaa vya kompyuta na simu janja ambazo tunazitumia leo hii. Au watu kama albert Einstein ambao ni maarufu kwenye ulimwengu wa fizikia. Kama hawawa tu wametumia uwezo chini ya asilimia kumi tu na siyo zaidi ya hapo, je, unadhani wewe umetumia uwezo kwa viwango gani. Ukweli ni kwamba unaweza ukawa haujatumia uwezo wako zaidi ya asilimia kumi.
Kwa hiyo basi, kama hujatumia uwezo wako kwa zaidi ya asilimia kumi halafu hapa njiani kinatokea kitu ambacho kinazuia uwezo wako, maana yake, unaenda kukwama zaidi ya hapo. Unachopaswa kufanya sasa hivi ni kuhakikisha kwamba umeondoa kikwazo chochote kile ambacho kinakuzuia wewe kuweza kutumia uwezo wako kwa viwango viikubwa. Badala yake unapaswa kuweka mazingira ambayo yanakuruhusu wewe kuweza kutumia uwezo wako kwa viwago vya hali ya juu kabisa, hivyo, basi ni jukumu lako kuanzia leo hii kuhakikisha kwamba upo kwenye mazingira ambayo yanakuruhusu wewe kuweza kutumia uwezo wako kwa viwango vya hali ya juu kabisa.
Swali muhimu unalopaswa kujiuliza siku ya leo ni je, nipo kwenye mazingira mazuri ya kutumia uwezo wangu kwa viwango vya hali ya juu. Je, mazingira haya yanaruhusu mimi kuweza kutumia uwezo wangu kwa viwango vya hali ya juu. Kama mazingira yako hayaruhusu wewe kuweza kutumia uwezo wako kwa viwango vya hali ya juu basi ni muda sasa wa kubadili hayo mazingira, na kama huwezi kubadili hayo mazingira basi unachopaswa kufanya ni kuhama kwenye hayo mazingira ili uweze kukaa kwenye mazingira ambayo yanakusapoti wewe kuweza kutumia uwezo wako kwa viwango vya hali ya juu.
Rafiki yangu labda tu nikwambie kitu. Utakaopokuwa umefikia umri wa uzee. Utakachojutia siyo wewe kutumia uwezo wako kwa viwangao vya hali ya juu. Bali utajutia kwamba hukuweza kutumia uwezo wako kwa viwango vya hali ya juu. Ndiyo maana leo hii ni kazi yako ni kuhakikisha kwamba umeutumia uwezo wako.
Sitaki siku moja ujutie kwamba hukuweza kutumia uwezo wako kwa viwango vya hali ya juu. M uda mzuri wa kutumia uwezo wako kwa viwango vya hali ya juu ulikuwa ni pale ulipopata akili. Ila muda mwingine mzuri zaidi ni sasa. Kwa hiyo, kama ulikuw abado huijaanz akutujia uwezo wako kwa viwango vikubwa, muda ni sasa. Anza kuutumia huwezo wqako huu kwa viwango vikubwa.
Na ukweli ni kwamba unapotumia uwezo wako siyo kwamba unakuwa unawanufaisha watu wengine tu. Bali wewe pia unakuwa unazidi kunufaika zaidi.
Uwezo tulionao ni kama misuli, kadiri unavyokuwa unautumia uwezo wako ndivyo unakuwa unazidi kuimarika zaidi na zaidi na kuongezeka. Kama ilivyo kwa misuli, kadiri unavyofanya mazoezi, ndivyo misuli yako inavyozidi kuimarika na kuwa bora zaidi. Kwa hiyo, kazi yako kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kwamba unautumia uwezo wako.
Lakini pia kutumia uwezo wako kunakupa ridhiko la moyo. Yaani, unakuwa unafanya kitu roho inapenda, wakati huohuo unakuwa na utulivu wa moyo na akili,. Hivi kwa mfano utajisikiaje kama wewe utakuwa mmoa wa watu ambao wameutumia uwezo wao vizuri na wana ridhiko kuuubwa la motyo na akili? Ni wazi kuw autajisikia vizuri sana. Kwa hiyo basi rafiki yangu, hakikisha kwamba unaanza kuutumia uwezo wako mara rmoja.
Kitu kingine kuhusu kuutumia uwezo wako ni kwamba unakuwa mbunifu. Kadiri unavyoutumia uwezo wako ndiyo unavyozidi kuwa mbunifu zaidi na zaidi.
Na kitu kingine muhimu sana kuhusu kuutumia uwezo wako ni kwamba, inakupa nafasi ya kuwasaidia wengine kutumia uwezo wao pia. Maaana kuna wau wataona namna unavyotumia uwezo kwako, na watu hao watakuywa tayari kujifunza na kutaka kujua ni kwa namna gani ambavyo wanaweza kutumia uwezo wao pia. Sasa kwa jinsi hiyo, utaweza kuwasaidia kwa kuwaabia kwamba mnaweza kutumia uwezo mlionao kwa viwango vikubwa kwa kufanyamambo yafuatayo.
Kish utawaorodheshea mambo yote ambayo wanapaswa kufanya ili kuweza kutumia uwezo wao.lakini pia kwa uwa umeshafanyia uwezo wako kwa viwango vikubwa, utakuw unajua kila kitu ambacho wanapaswa kufanyia kazi ili kuweza kuutumia uwezo wao kwa viwango vya hali ya juu sana.
Hivyo rafiki yangu, kazi yako ni moja tu. Ni kuhakikisha kwamba umeutumia uwezo wako. Kwa sababu utakuwa mtu mwenye faida pale tu ambapo utaaamua kuuutmia uwezo wako kuliko pale ambapo utakuwa hujaweza kutumia uwezo wako.
Hayo ndiyoambayo nilitaka kukushirikisha siku ya leo rafiki yangu wa ukweli. Naamini sana leo umewezaakundondooka na kitu kikubwa sana kwenye makaal hii.
Nikutakie wikendi njema kabisa.
kabla hujamalizia kusoma makala hii nakuomba kitu kimoja tu. Na kitu hiki ni kwamba uwashirikishe wenzako makala hii ili nao waweze kuisoma na kunufaika nayo.
Asante sana.
Makala hii imeandikwa name rafiki yako
Godius Rweyongeza
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwangu kwa kupatanakala za vitabu vyangu. Na vitabu vyangu unawezakuvipata mtandaoni kupitia hapa
Au unaweza kuwasiliana na 0684408755 sasa ili uweze kupata nakala zako
Asante sana na uwe na siku njema.
Hakikisha umepata kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, kitabu hiki kitakupa mwongozo kamili wa jinsi ya kutumia uwezo mkubwa bila kukwama wala kurudi nyuma.
Kupata nakala yako, tuwasiliane kwa 0684 408 755 sasa