Rafiki yangu mpedwa salaam, hongera sana kwa siku hiii ya leo. Siku ya leo ningependa tu kukushirikisha kauli moja ambayo unapaswa kuwa unajiambia kila siku kwenye biashara na kwenye kitu chochote kile unachofanya.
Mara nyingi ukianza kufanya kazi au kitu chochote huwa wanatokea watu ambao wanakuwa na maoni ya kukushauri juu ya nini cha kufanya au nini ambacho haupaswi kufanya. Sasa kitu hiki kitakufanya usikilize miluzi mingi ambayo mwisho wa siku hiyo miluzi itakupoteza. Sasa ili kwenda vizuri nashauri kitu kimoja kwako
Na kitu hiki ni kwamba ni bora nife nikiwa nafanya kile ambacho ninapenda kuliko kufanya kile ambacho ninapangiwa na watu wengine. Hivyo, basi fanya kile ambacho wewe wenyewe unapenda na siyo kile ambacho watu wengine wanakupangia kufanya.
Ni bora ufe ukiwa unafanya kile ambacho wewe mwenyewe unapenda kuliko kufanya kile ambacho watu wengine wamekupangia kufanya.
Nakutakia siku njema sana
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
Unaweza kuwasiliana na mwandishi wa makala hii kwa simu 0755848391
Kupata vitabu vyake, unaweza kuwasiliana naye kwa 0684408755
Karibu sana