Kheri ya MWEZI WA SEPTEMBA


Siku zinaenda balaa, ni kama jana tu nakumbuka watu walivyokesha wakiusubiri mwaka mpya. Watu walivyokuwa na mbwembwe za mwaka mpya na mambo mapya, hivi kwenu haya mambo yapo, au ni ushamba wa huku nilipo tu!

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu wengi ambao huwa wanaweka malengo. Huwa wanayasahau malengo yao kufikia januari 19, je, wewe malengo yako bado unayakumbuka?

Katika ujumbe wangu wa kukutakia  kheri ya mwezi mpya siku ya leo,. Napenda pia kukumbusha kuwa tumebaki na siku 120 mwaka huu uishe.

Hizi siku 120 usizichukulie poa na wala usianze kusema kwamba, ngoja mwaka huu uishe najipanga kwa ajili ya mwakani. Ukweli ni kwamba mwaka huu bado unapaswa kufanya makubwa. Siku 120 zilizobaki ni nyingi sana. Anza kujituma ndani ya hizi siku 120 kuhakikisha kwamba kila siku unafanya kitu cha tofauti.  Chagua kitu kimoja, kisha jisukume kufanya hiki kitu kwa siku 120 zijazo bila ya kurudi nyuma. Ukiweza kufanya kitu kimoja kwa siku 120 zijazo ni wazi kuwa kwanza utajijengea nidhamu, lakini pia kuna kitu ambacho utaweza kufanikisha ndani ya huu mwaka ambacho miakamingi ijayo utajivunia sana.

Siku 120 ni sawa na mhura mmoja wa chuo kikuu. Ndani ya mhura mmoja mwanachuo anatarajiwa kuwa ameelewa mada ambazo zinafundishwa kwa undani.

Na mhula mmoja ni kipimo kinachotumika kumpima mwanachuo kuona uelewa wake.

Wewe pia jipe huu mhula mmoja wa chuo kupambana.

Mhura wa kufanyia kazi malengo yako hata kama ulikuwa uliyaweka pembeni au ulitulia. Unataka kuandika kitabu, una mhura huu mmoja wa kufanya hivyo.

Unataka kuongeza kipato chako, una mhura huu mmoja wa kufanya hivyo.

Unataka kuweka akiba, utumie mhura huu kuweka akiba bila yakuacha

Unataka kujiondoa kwenye dimbwi la mawazo na sonona inayokusumbnua, una siku 120 za kufanya hivyo.

Ndani y a hii miezi minne zima kila kitu ambacho hakiendani na lengo lako kuu, kisha juhudi zako zote ziwekeze kwenye lango lako kuu. Kamwe rafiki yangu usikubali kurudi nyuma wala kuyumbandani ya hiki kipindi, huu ni muda wako wa kung’aa. Hakikisha unautumia kung’aa kweli.

Kama unataka usimamizi wa karibu ndani ya hiki kipindi cha siku 120 zijazo, njoo kikashani nitakusaidia kukushika mkono ili ufanyie kazi lengo lakompaka lifanikiwe. Namba ya kuwasilialina nami ni 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X