Siri ya mafanikio ya kweli ni hii hapa


Usiache kufanya jambo lako kwa sababu huoni matokeo ya muda mfupi. Badala yake kaza. Endelea kupambana kwa muda mrefu

Kuna watu wengi hawafanikiwi kwenye maisha kwa sababu ya kujaribu vitu vingi kwa muda mfupi na kuacha.

Sikiliza chagua kitu kimoja
Kifanye kwa uhakika
Kifanye kwa muda mrefu bila kuacha.
Bobea kwenye hicho kiasi kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kufanya kitu hicho kwa ubora kama wewe

Kinyume chake kitakufanya ufeli.
Kama
Utafanya kila kitu.
Ukakifanya kwa mguu mmoja ndani na mwingine nje.
Ukafanya kwa muda mfupi na kuacha na kwenda kufanya mengine na yenyewe ukayafanya kwa muda mfupi mfupi huku ukiacha.
Ukayafanya bila ufanisi.

Mwisho wa siku utaishia kuwa na maisha ya kawaida. Na haya ndiyo maisha ya watu wengi.

Nakwambia ufanye kitu kimoja kwa muda mrefu nikiwa na sababu za msingi kabisa.
Moja ya sababu hizo ni kwamba kuna watu ambao mwanzoni wanakuwa wanakufuatilua, japo kwenye kukufuatilia kwao hawachukui hatua.

Ni kama wanakuwa wanaangalia kama unabeep au unafanya kweli. Na pale unapothubitisha bila shaka kuwa umedhamiria kufanya ulichochagua, basi huwa wanaanza kukufuatilia kwa ukaribu na hata kuwa wateja wako

Mtu anaweza kukupuuza mara ya kwanza.
Mtu anaweza kukupuuza mara mbili ila hawezi kukupuuza mara zote.

Huvyo, kuendelea kwako ndiyo njia pekee itakayokufikisha kule unapotaka


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X