Tabia za kimasikini unazopaswa kuachana nazo sasa hivi.


Rafiki yangu mpendwa salaam, leo ningependa kukwambia tabia za kimasikini ambazo unapaswa kuachana nazo. Achana na tabia hizi kwa manufaa yako.

Kwanza ni vitu ambavyo vinapoteza nguvu zako. Hivi ni vitu vyote ambavyo vinapoteza nguvu zako vitu kama pombe, sigara, ulevi wa aina yoyote, kula vyakula vya hovyo na mambo mengine kama hayo.

Pili, ni tabia ya kutumia kiasi kikubwa kuliko unavyoingiza. Hii ni tabi anyingine ambayo inaenda kukuanya wewe kuwa maskini maisha yako yote. Ibadili tabia hii kwa kujiwekea tabia ya kuwekeza, kuanzia leo hii.

Tatu, tabia ya kuwa tagemezi. Kumbuka kwamba maisha ni wajibu wako. Ukishinda ni juu yako na ukishindwa ni juu yako. Hivyo, beba jukumu la maisha yako.

Nne,  ni tabia ya kuzembea kazi. Achana kabisa na tabia ya kuzembea kazi yako, anzak uchapa kazi yako kwa bidii kubwa. na

Tano, ni tabia ya kutojiongeza. Maskini wengi wanasubiri waambiwe cha kufanya ndiyo wafanye. na hata baada ya kuambiwa hawafanyi kama wanavyopaswa kufanya, ni mpaka wasimamiwe ndiyo wanafanya. Akitoka msimamizi, basi wao wanaanza kuzembea. wewe usiwe mmoja wao, penda kuchapa kazi tena kwa bidii hata kama hakuna mtu wa kukusimamia.

Kwenye kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA nimeeleza tofauti 50 kati ya matajiri na masikini. Hakikisha unapata kitabu hiki kwa manufaa yako. softcopy ni 10,000 tu. kukipata wasiliana na 0684408755

Karibu sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X