Ukiuza vitabu vyako vyote ambavyo umewahi kununua utapata shilingi ngapi?
Leo kuna mtu nilikuwa naongea naye, akaniambia vitabu ambavyo nimewahi kununua, nikiviuza vyote naweza kujenga nyumba kubwa ya kifahari.
Hiki kitu kikawa kinanitafakarisha kuhusu wewe …
Hivi wewe ukiuza VITABU vyote ambavyo umewahi kununua unaweza kufanya nini?
Vitabu vinakufanya uone mbali hata wewe ni mfupi?
Kila mwezi jiwekee utaratibu wa kununua walau kitabu kimoja tu. Kisha kisome hicho kitabu, ninakuhakikishia baada ya mwaka utakuwa umeweza kufanya makubwa sana.
Vitabu unavyosoma vitatuonesha aina ya mtu wa siku zijazo. Ndiyo maana, Charles Tremendous Jones alisema kwamba miaka mitano ijayo utakuwa jinsi ulivyo, isipokuwa kwa vitu viwili tu. Vitabu unavyosoma na watu unaokutana nao.
Jiwekee utaratibu wa kununua na kusoma vitabu vizuri.
Ukikutana na kitabu kizuri kirudie kukisoma mara kwa mara bila kuchoka.
Kisha kitumie kitabu kwa kufanyia kazi kile unachojifunza.