Kama Hujisikii Kufanya Kazi


Huwa inatokea kwamba ninaanza kuandika huku nikiwa sijui ni kitu gani cha kuandika. Sijapangilia mada ya kuandika lakini muda huohuo napaswa kuandika na kuonesha kitu kwa watu wangu wa nguvu kama wewe hapo.

Na siku ya leo ni mojawapo.

Hata hivyo huwa ikitokea siku kama hii, kitu cha pekee ambacho huwa natakiwa kufanya siyo kuacha kuandika na kusubiri kwamba nitaandika kesho au wakati mwingine ambapo nitakuwa na kitu cha kuandika au hamasa ya kuandika, badala yake huwa napawa kukaa chini na kuanza kuandika, kwa maana muda mwingne hamasa huwa inakuja nikiwa naandika au kitu cha kuandika naweza kukipata nikiwa naandika kuliko pale ninapokuwa siandiki.

Si unajua huwezi kujikwaa kama hutembei Inawezekana wewe ukawa huandiki kama mimi. Lakini wakati mwingine ukawa hujisikii kuwa na hamasa ya kufanya kile kitu ambacho unatakiwa kufanya, hapa kuna vitu vitano ambavyo unapaswa kufanya unapokuwa kwenye hiyo hali..

KITU CHA KWANZA NI KUANZA KUFANYA HICHO KITU

Hiki ni kitu cha kwanza kabisa ambacho unapaswa kuanza nacho, anza kufanya kitu hata kama kwa wakati huo hujisikii kukifanya. Unaweza kwa nje ukawa hujisikii kuwa na motisha na nguvu ya kufanya hicho kitu, ila ile unapoanza kukifanyia kazi kile kitu unajikuta kwamba unapata hamasa ya kufanya zaidi hicho kitu na unajikuta unakuwa na ari. Hiki ni kitu ambacho wewe kwa upande wako unakuwa unahitaji. Kumbe anza kufanya kitu hata kama hujisikii wakati mwingine motisha na ari huwa inakuja ukiwa unafanya kuliko pale unapokuwa hufanyi kitu chochote.

KITU CHA PILI NI KUJIKUMBUSHA NDOTO ZAKO KUBWA

Kujikumbusha ndoto na malengo yako makubwa ni njia nyingine nzuri yaw ewe kurudi kwenye ari ya kufanyia kazi malengo yako. Kama hujisikii kufanya kitu, kaa chini na andika malengo yako na ndoto zako za muda mrefu. Kisha andika ni kitu gani kimoja ambacho unaweza kuanza kufanya sasa kikakupeleka wewe kwenye kufanikisha malengo yako ya sasa

TATU NI KUJIFUNZA

Kusoma, kusikiliza au kuangalia video za hamasa kutoka kwa watu ambao wanafanya vitu na kupata matokeo inaweza kuwae ni njia nyingine ya kukufanya uendelee kukaa kwenye mstari kila mara, kazi yako kubwa kutoka inakuwa siyo tu kujifunza bali kufanyia kazi kile ulichojifunza kwa vitendo ili uweze kupata matokeo.

Rafiki yangu, inawezekana kwa sasa hauna hamasa ya kufanya kitu ambacho unapaswa kufanya. Haupasswi kukaa tu na kusubiri upate hamas aya kuanza kufanya kile kitu. Unachotakiwa kufanya ni kuingia ulingoni na kuanza kufanya hicho kitu. Ni kupitia kufanya, ndiyo utajikuta kwamba umeweza kukifanya.

Tena siku ambayo muda mwingine unakuwa hujisikii kufanya kitu, ndiyo siku ambayo unakuta kwamba inatokea kuwa siku bora kwako kuwahi kutokea kwenye kufanya kazi. Unajikuta kwamba umeweza kufanya kazi bora kabisa.

Hili linatokeaje, linatokea kwa wewe kuanza na kuchukua hatua ya kwanza ambayo ni kuanza kufanyia kazi kile ambacho mwanzoni ulikuw ahata hujikii kufanya.

EBU KWENYE MAONI, NIWEKEE MAONI YAKO, NIJUE KAMA IMEWAHI KUKUTOKEA SIKU KAMA HII KWENYE MAISHA YAKO NA NI KITU GANI AMBACHO ULIFANYA

MPAKA WAKATI MWINGINE, CHEERS

NB: Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao bado hawajapata nakala ya kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA,basi ifanye leo kuwa siku yako ya kupata nakala ya kitabu hiki cha kipekee. Naam, kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. Halafu kupata nakala ya kitabu hiki ni rahisi sana.

Nakala ngumu ni 20,000/-

Na nakala laini ni 10,000

Kupata nakala mojawapo hapo juu. Unalipia kwenda namba 0684408755

Changamka ufanye hivyo sasa

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Unaweza ujifunza zaidi kutoka kwa GODIUS Rweyongeza kwa kujiunga na watu wake wa nguvu ambao huwa wanapokea maandiko yake kupitia barua pepe

Jiunge hapa

Kuwasiliana moja kwa moja na Godius Rweyongeza, tumia godiusrweyongeza1@gmail.com

Kupata vitabu wasiliana na 0684408755

Kujifunza uandishi: 0687848391

Karibu


One response to “Kama Hujisikii Kufanya Kazi”

  1. Mie Kuna wakati najiskia kitabia ya Kivu vivu yakuhanza kazi, na ingine inayo nirudisha nyuma sana ni hali yakukwama kwenye harakati zangu, yaani yakutofanyikiwa kabisa, mie najiusisha sana na mambo ya madini yaani dhaabu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X