Kishiria kuwa umechelewa kufanya maamuzi


Rafiki yangu, kila siku kuna maamuzi ambayo tunatakiwa tufanye, yanaweza kuwa ni maamuzi ya nani uwe naye kwenye mahusiano, maamuzi ya biashara gani ufanye, maamuzi ya sehemu gani uende kutembelea. Maamuzi ya aina gani ya matangazo ufanye. Maamuzi ya nani umwajiri, nani umwondoe kazini au nani umpandishe cheo. Maamuzi ya shule gani mwanao asome au gari gani ununue na mengine mengi.

Kwa kuwa kuna maeneo mengi ya kufanyia maamuzi, siku ya leo ningependa tu kukwambia kuwa kama unafanya maamuzi hasa kwenye biashara ukiwa na uhakika wa asilimia 100 basi ni wazi kuwa unakuwa umechelewa. Yaani, umesubiri kila kitu kiwe sawa sawia.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X