Kuanguka ni kiashiria kuwa kuna kitu unafanya


Kuanguka siyo tatizo, kuanguka ni kishiria kwamba kuna kitu unafanya na ndiyo maana unakutana na vikwazo. Kumbe kuanguka kwako usikuone kama kigezo cha wewe kutoendelea mbele. Bali kuone kama sehemu ya wewe kuendelea kusonga mbele ili kuja kufanya makubwa zaidi.

Kadiri unavyokua, maanguko yako yanakuwa makubwa zaidi. Na yanajulikana kwa watu wengi zaidi kuliko pale unapokuwa chini, lakini hili lisikurudishe nyuma wala kukufanya ushindwe uweze kufanyia kazi malengo na ndoto zako. Bali hili liwe ni kama chachu ya wewe kuweza kufanya makubwa zaidi

Kwa sababu ukiendelea kubaki hapohapo ulipo, itakuwa ni vigumu kwako kuweza kufanya makubwa zaidi.

Wengine wanaogopa kuchukua hatua kwa sababu wanalinda heshima, labda ameajiriwa na anaogopa kwamba akianzisha biashara itafeli. Ukweli ni kuwa kulinda heshima ni sawa na timu inayolinda goli wakati wa mechi. Kama wachezaji hawatatoka kwenda kushambulia. Tena kushambilia kwa kiingereza kuna gumu kidogo  to make an offense, . Kama wachezaji hawatatoka kwenda kushambulia, ujue wazi kuwa timu hiyo haitafunga.

Lakini uwezekano wa timu hiyo kufungwa ni mkubwa sana.

Kama huchukui hatua yoyote ile kwa kuogopa kushindwa, unakuwa huna tofauti na mtu ambaye analinda lango. Kazi yako, siyo kulinda lango, bali kushambulia mara kwa mara kadiri unavyoweza. Kadiri unavyoshambulia ndivyo ambavyo unaongeza uwezekano wa wewe kuweza kufunga zaidi.

Siku ya leo nataka uondoke na vitu viwili vikubwa

Kwanza fahamu kuwa kushindwa siyo tatizo, bali kushindwa kuchukua hatua na kuogopa kushindwa ni kikwazo na tatizo pia.

Pili, nataka ufahamu kuwa  mara zote unapaswa kuwa kwenye mwendo wa kushambulia. Usilinde lango, usilinde heshima. Wewe shambulia tu hata kama utashindwa, utapata heshima zaidi kwa kushambulia kuliko kulinda lango

Mpaka siku nyingine, uwe na siku njema sana.

By the way nimeandika vitabu  viwili ambavyo kwa siku ya leo ni muhimu sana kwako uvipate. Kitabu cha kwanza ni kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA, na kitabu kingine ni kitaub cha NYUMA YA USHINDI: Kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa. Kuapata nakala za vitabu hivi tuwasiliane kwa 0684408755 sasa

Mpaka kesho, mimi nakutakia siku njema kwako


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X