Wewe unafahamika Kwa kitu Gani ?


Moja ya uamuzi unaohitaji kufanya ni Uamuzi wa namna unavyotaka ufahamike kwenye maisha Yako. Nimekuwa nikisisitiza hiki kitu mara Kwa mara, lakini cha kushangaza ni kuwa Watu wengi wamekuwa Bado wanarudia kufanya makosa yaleyale Kila mara.

Ngoja nikwambie KITU, watu wengi unaowafahamu, huwafahamu Kwa sababu wanafanya Kila kitu au walikuwa wanafanya Kila kitu, bali unawafahamu Kwa sababu walibobea sehemu Moja.

  1. Iwe ni viongozi wa kiroho kama Budha, Yesu na Mtume Muhammad
  2. Au wanasiasa kama Nyerere.
  3. Au wanamuziki
  4. Wanamichezo na hata waandishi

Nyerere anafahamika kama mwalimu, lakini impact yake haukuwa kwenye kufundisha, kwake ualimu umebaki kuwa cheo Cha heshima tu, ila impact yake ilikuwa kwenye siasa.

Ndiyo maana mwaka 1955 aliachana na ualimu Ili aingie kwenye siasa Kwa sababu huko ndiko alitaka kuacha alama.

Ualimu ulikuwa unamlipa. Kwa lugha ya Leo tunaweza kusema alikuwa anapata maokoto mazuri tu Kwa ajili ya kuendesha maisha yake, Tena kipindi hicho ambacho Ajira zilikuwa ni adimu.

Lakini aliamua kuachana na Ajira Ili na kuingia kwenye siasa, Kwa sababu aliona alama yake kubwa ataiacha kama atakuwa kwenye siasa kuliko akiwa mwalimu.

Wakati mwingine inaonekana vigumu kuweka nguvu sehemu moja hasa pale ambapo vitu vyako vidogo vidogo unavyofanya vinapokuwa vinakuingizia maokoto kidogokidogo. Ila ukweli ni kuwa hiki kitu ndicho kitakupoteza pia. Maana haya maokoto kidogo ndiyo yatakunyina pesa za maana laiti kama ungewekeza muda na nguvu zako sehemu Moja na kuikuza. Ni ukweli kuwa ungeweza kupata matokeo makubwa zaidi.

Jipe muda wa kuwekeza kwenye ndoto Yako kuu na kuachana na vitu vingine vyote unavyofanya Kwa Sasa.

Inaweza isikulipe Kwa Sasa ila itakulipa baadaye.

Makala ya Leo imeandikwa na Godius Rweyongeza
Whatsap: 0687848391
Calls & SMS: 0755848391

Jifunze zaidi Kwa Godius Rweyongeza Kwa kutembelea www.songambele.co.tz

Mpaka wakati mwingine. Tchao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X