Habari ya asubuhi upande wa huko
Hii ni wiki ya huduma kwa wateja. Na nimeona nikupe taarifa muhimu sana rafiki yangu. Na taarifa hii ni kwamba wiki hii una kila sababu ya kuwasiliana na wateja wako.
Mpigie hsimu hata mteja mwambia kwamba hii ni wiki ya huduma kwa wateja na nimepiga simu kwa ajili ya kukusalimia.
Mpigie hata mteja kumuuliza kama anaweza kuweka oda ndani ya hii wiki ya huduma kwa wateja.
Toa hata ofa kwa wateja wako.
Tuma hata ujumbe kwa wateja kuwasalimia
Omba hata maoni kwa wateja wako
Waambie wateja kuna mzigo mpya
Fanya chochote kile ndani ya hii wiki ya huduma kwa wateja kwa ajili ya wateja kuhakikisha unakuwa nao karibu. Asibaki hata mmoja ambaye hatasiki chochote kutoka kwako ndani ya hii wiki
Uwe na wiki njema sana
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
Email: songambele.smb@gmail.com