Jinsi ya kupunguza najuto yako utakapokuwa umezeeka


Moja ya changamoto kubwa ammbayo huwa inawakuta watu ambao wanakuwa hawafanyii kazi malengo na ndoto zao ni kwamba wanapofikia mwisho wa maisha yao basi wanakuwa na majuto mengi ambayo yanawaandama kutokana nay ale ambayo hawakuweza kufanyia kazi. Sasa wali kubwa ambalo unaweza kuwa unajiuliza ni kuwa je, kuna namna ambavyo naweza kupunguza haya majuto kwenye maisha yangu? Je, kuna namna ambavyo naweza nisije kuwa na majuto kabisa?

Ili kujibu haya maswali ni lazima kwanza tujue ni kitu gani ambacho huwa kinasababisha watu kuwa na majuto

Kwanza ni kufanya yale ambayo hawapendi.

Pili ni kutotumia uwezo wao

Tatu ni kutosimamia ukweli

Nne, ni kutochukua hatua na kujituma zaidi hasa  wanapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Sasa kujua vitu ambavyo huwa vinasabahisha majuto miongoni mwa watu ni hatua moja kuwa, ila sasa baada ya kuijua hii hatua, kinachofuata ni kuchukua uamuzi wa  wa kuahikisha kuwa mwisho wa siku unakuwa hauna majuto kwenye maisha yako. Fanya kinyume na hivyo vitu yaani

Fanya yale unayopenda kufanya

Fanya yale unayoona ni sahihi

Simamia ukweli

Tumia uwezo wako bila kuubana

Ukiweza kufanya hivyo, ni ukweli ulio wazi na usiopingika kuwa mwisho wa maisha yako hautakuwa na majuto, bali utakuwe umeweza kufanikisha makubwa pia

Kwa leo inatosha, nikutakie siku njema sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X