Mambo kumi yatakayokusaidia kulianza juma hili ukiwa mbele ya watu wengine


  1. Kwenye kila hatua unayofikia, bado kunakuwepo na hatua nyingine kubwa mbele yako ambazo unaweza kupiga, kwa hiyo usijizurie kupiga hatua kwenye Maisha yako kwa sababu ya mafanikio ya muda mfupi ambayo unapata. Badala yake kila mara jiulize ni kwa namna gani naweza kutumia matokeo ya sasa kwenda mbele Zaidi.
  2. Unachohhitaji wewe ni kuendelea mbele hata kama unapitia kwenye changamoto. Kitendo cha wewe kuendelea mbele kitaonesha kuwa wewe ni shuujaa
  3. Watu wanaofanya vitu vya tofauti siyo kwamba wana muda mwingi wa kutosha kama unavyofikiri, nilichogundua ni kwamba mtu yeyote wa kawaida anayeweza kupangilia ratiba yake ya kila siku na akaifuata hiyo ratiba, anaweza kufanya makubwa kuliko mtu  anayesubiri kuwa na muda wa kutosha ili afaie kazi anachotamani.
  4. Kuwa na ndoto kubwa ni kitu kmoja, ila kufanyia kazi ndoto zako kubwa ni kitu kingine. Wewe kuwa upande wa kufanyia kazi ndoto zako.
  5. Ndoto yako kubwa kwa vyovyote vile inahitaji fedha, kuwa mtumiaji mzuri wa fedha, wekeza, na kila fedha inayoingia mfukoni mwako itumie vizuri kwa manufaa yako ya sasa na baadaye.
  6. Kama unataka kuishi Maisha ya kawaida, fanya vitu vya kawaida, kama unataka kufanya mambo ya tofauti, fanya vitu vya kawaida katika namna ambayo siyo ya kawaida.
  7. Mambo mengine yote yanaweza kusubiri, ila usisubirishe ndoto zako anza kuzifanyia kazi ndoto zako. anza kuzifanyia kazi ndoto zako hata kwa udogo.
  8. Kuna vitu viwili ambavyo kama bado hujavifanikisha basi unapaswa kuendelea kupambana mpaka kieleweke, endelea kupambana bila ya kurudia nyuma. Kitu cha kwanza ni kuwa na uwekezaji ambao unakuingizia fedha hata kama umelala na hapa siongelei fedha za kawaida, bali naongelea fedha za kuishia Maisha unayotaka , kama bado hujafikia hiki kiwango, basi usilale Rafiki yangu, endelea kupambana mpaka kieleweke.
  9. Kitu cha pili ambacho kama hujakifikia ni kuwa biashara ambayo inaweza kujiendwesha yenyewe bila ya kukuhitaji wewe. Kama bado hujafikia kwenye hivi viwango, basi unapaswa pia kuendelea kupambana bila ya kurudi nyuma mpaka kieleweke.
  10. Ishi Maisha yako, usiige Maisha ya watu wengine, unapoanza kuishi Maisha ya watu wengine, moja kwa moja unakuwa unajinyima fursa ya kuwa wewe halisi na kuonesha kile ambacho wewe mwenywewe unaweza kufanya..

Hayo kwa leo yanatosha. Nikutakie mwanzo mwema wa juma hili hapa.

Kila la kheri na waslimia sana Rafiki zako walio karibu na wewe.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X