Mara kwa mara watu wamekuwa wanatafuta hamasa ya kufanya kitu. Ukweli ni kuwa huhitaji hamasa pekee ili kufanikisha lengo na ndoto yako kubwa. Bali unahitaji matendo ili uweze kufanyia kazi malengo na ndoto zako ziweze kufanikiwa.
Nakwambia hivi kwa sababu hamasa huwa haidumu, hamasa ni kitu cha muda mfupi ambacho kinapotea. Hivyo ili ufanikishe malengo na ndoto zako kubwa ulizonazo unahitaji zaidi ya hamasa. Unahitaji matendo
Wakati mwingine hujisikii kama kufanya kitu chochote kile. Lakini unapaswa kujisukuma kwa sababu ukisubiri hamasa pekee ili ufanyie kazi ndoto zako, ukweli ni kuwa hamasa hiyo itachelewa sana.
Leo hujisikii kama una hamasa. Sikiliza, fanya kitu kimoja tu. Fanya kile kitu unachopaswa kufanya hata kama huna hamasa. Hamasa itakuja njiani, na hata kama hamasa haitakuja, utakuwa umeweza kukifanya hicho kitu.
Kwa leo nadhani ujumbe umetosha sana.
Kikubwa ni wewe kuufanyia kazi
Kupata nakala za vitabu vyangu, basi wasiliana na 0684408755 karibu sana.