Je, kuna ulazima wowote ule wa kuandika majukumu yangu chini naweza kuyakumbuka?


Kwenye makala ya jana nilikwambia kwamba unapaswa kuandika majukumu yako yak la siku. Unapaswa kuhakikisha kwamba umeyaandika chini. Lakini., Inawezekana wewe ukawa na kumbukumbu nzuri, hivyo ukajiambia kwamba sipaswi kuwa naandika vitu vyangu chini.

Siku ya leo nipo hapa kukwambia kuwa hata kama una kumbukumbu nzuri. Hata kama unayesoma hapa ni profesa. Bado unapaswa kuandika chini majukumu yako utakayoyafanya ndani ya siku husika. Huandiki chini m ajukumu yako ya siku husika kwa sababu utasahau, bali unaandika chini ili uweze kuipa akili na kichwa chako nafasi ya kufikiria mambo mengine ya maana zaidi.

Hivyo, ile nguvu ambayo ungeitumia kwenye kukumbuka ratiba yako ya siku, unaitumia kwenye kwenye mambo mengine yatakayokupa matokeo makubwa zaidi.

Sijui umenielewa hapo? Ee, usije kusema ooh, unajua mimi nina kumbukumbu kubwa bwana sihitaji ratiba. Hapana,  andika chini, ratiba yako.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X