Rafiki yangu mpendwa salaam, bila shaka unaendelea vizuri.
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini unakuwa unapoteza muda kwenye siku yako? Unajua kwa nini hili linatokea? Moja ya kitu kinachokufanya upoteze sana muda wako ni kwa sababu, hujapangilia vizuri siku yako. Yaani, chochotfe kile kinachokuja mbele yako wewe unafanya. Ukweli ni kuwa unapoianza siku yako, unapaswa kuutumia muda wako kwenye kuipangilia siku yako.
Ndiyo, andika saa kwa saa kitu ambacho unaenda kufanyia kazi ndani ya siku husika.
Kisha fuata hiyo ratiba yako.
Hiki kitakusaidia kuepukana na muda mwingi ambao ungeupoteza ndani ya siku yako. Lakini pia kitakusaidia kuiendea siku yako katika namna ambayo itakuzalishia matokeo.
Kwenye ratiba yako weka vitu ambavyo utafanya na vitakuletea matokeo. Kama kitu hakitaleta matokeo sasa au siku zijazo, kiondoe. Kipaumbele chako kiwe ni yale majukumu yako ya muhimu tu.
Sijui umenielewa.
Ebu anza leo. Ni kwa namna gani unaenda kupangilia ratiba yako siku ya leo? Ni vitu gani ambavyo unaenda kuondoa kwenye maisha yako ambavyo umekuwa unafanya ila havina manufaa?
Nitumie ujumbe whatsap kwa 0755848391
Emai: godiusrweyongeza1@gmail.com
Kila la kheri
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Kujifunza kuhusu uandishi wa makala. BONYEZA HAPA