Kitu muhimu unachopaswa kukifanya unapokuwa unakutana na mtu


Niwe mkweli, hiki kitu mwenyewe kimekuwa kinanipa shida sana. Watu wengi wanaomba kuonana namimi halafu muda mwingine wanakuwa hawajajipanga. Na muda mwingine wanaomba tu kuonana na mimi ilimradi…. Lakini pia mimi siwaambii muda ambao nitaweza kuwa nao.

Nimejifanyia tafakari kwa watu wengi ambao wameomba kuonana na mimi ndani ya mwaka 2023, nimegundua kitu hiki kimejirudia sana. Hivyo, nimeamua mwaka 2024, ninaenda kufuata utaratibu wangu kama ifuatavyo.

Kabla ya kuonana utaniambia tunataka tuongee nini.

Kama kuna gharama ambazo utakuwa unapaswa kulipia utalipia mapema.

Halafu tutapanga muda wa kuonana na kikao hicho kitadumu kwa muda gani.

Ukichelewa, imekula kwako. Muda wako umeenda.

Usipofika kwa wakati na hakukuwa na taarifa mapema, basi muda wangu wa kuondoka ukifika nitaodnoka. Hili litanisaiaidia kuonana na watu wachache, ila ambao wako siriazi na ambao tutafanya mambo ya maana.

Nimejieleza mwenyewe leo hii, lakini pia na wewe angalia kwenye ratiba zako. Hivi kwa mfano, mwaka huu umekutana na watu wangapi? Je, ni muda kiasi gani umepoteza kwa vikao ambavyo havikuwa na tija?

Hilo liondoe kwenye ratiba zako. Mwaka 2024, usirudie kosa hilohilo, la sivyo litakukwamisha kusonga mbele.

Kama umenielewa gonga cheers, kisha mshirikishe rafiki yako makala hii aweze kusoma.

Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X