Kwenye maisha kuna makosa ambayo watu huwa wanafanya. Ila hupaswi kufanya makosa ya nanma hii mengi, maana kadiri unavyofanya makosa haya mengi, maana yake unakuwa unajiuzuia ile nafasi yaw ewe kusonga mbele na kuweza kfuanya makubwa zaidi. Sasa unajua ni kosa gani kubwa ambalo watu hufanya?
Kutojifunza baada ya kumaliza chuo.
Ile baada ya mtu kuhitimu na kurusha kofia juu, ndiyo anakuwa amerusha kila kitu. Yaani, hataki tena masuala ya kusikia sijui kuna vitabu au kitu gani. Ukweli ni kuwa kama unataka kufika mbali kwenye maisha kusoma kunapaswa kuwa sehemu ya maisha yako.
Nani amekwambia kwamba, ukijifunza kitu kimoja tu mara moja tu ndiyo unakuwa umebobea. Unapaswa kuendelea kujifunza kila siku bila ya kuacha. Kila siku, ya maisha yako iwe ni siku ya kujifunza.
Kiukweli ili ufanikiwe kwenye maisha unahitaji zaidi ya elimu ya darasani. Unahitaji kujifunza vitu vingi. Unahitaji kujifunza biashara, unahitaji kujifunza mauzo, unahitaji kujifunza kuongea mbele ya watu, unahitaji kujifunza uandishi na mengine mengi.
Soma na jifunze mara kwa mara. Iwe ni kupitia vitabuni, iwe ni kupitia kozi ambazo unaweza kusoma mtandaoni, kozi za kwenda sehemu na njia nyinginezo.
Ningependa nimalizie makala ya leo kwa nukuu inayosema kuwa, mtu ambaye hasomi, ni mzee hata kama bado ana miaka 20 na mtu ambaye anasoma na kujifunza ni kijana hata kama ana miaka 80.
Uwe na siku njema.