Usisubiri Mtu Yeyote Kuanza Kufanyia Kazi Ndoto Zako


  1. USISUBIRI YA MTU YEYOTE KUANZA KUFANYIA KAZI NDOTO NA MALENGO YAKO. Ndiyo unapawa kuwa na ndoto kubwa bila ya kusubiri mtu yeyote, ila ukweli ni kuwa ndoto kubwa na malengo makubwa bila ya kufanyia kazi, hayatakaa yatimie. Ndiyo maana unapaswa kuanza kufanyia kazi malengo na ndoto zako bila ya kusubiri ruhusa.

Kwenye andiko langu la Jana ee mtu mkubwa….niliandika kuhusu kuwa na ndoto kubwa. Ndiyo unapawa kuwa na ndoto kubwa bila ya kusubiri ruhusa ya mtu yeyote, ila ukwlei ni kuwa ndoto kubwa na malengo makubwa bila ya kufanyia kazi, hayatakaa yatimie. Ndiyo maana unapaswa kuanza kufanyia kazi malengo na ndoto zako bila ya kusubiri ruhusa.Kuifanyia Kazi ndoto Yako ndiyo habari mjini.
 
Huu ni upande wa pili wa shillingi. Upande wa kwanza ni KUWA NA NDOTO Kubwa upande wa pili unaosema baada ya kuwa na ndoto kubwa Sasa unapaswa kuzifanyia kazi.
 
Ebu pata picha kama Dunia yote ikibadilika Leo hii unaposoma hapa na Kila mmoja akaanza kuwa bize na ndoto zake.
 
Aliyekuwa anapiga umbea ukakuta ndiye Yuko bize na ndoto zake kubwa. Hataki utani, hataki umbea ila kipaumbele kwake ni kazi TU. Na kazi hiyo ni ndoto zake.
 
Baada ya kuwa umeonana na huyo mtu pata picha ukatoka hapo ukaenda kukutana na mwingine ambaye siku za nyuma alikuwa anakaa kaa tu bila kufanya kitu chochote, lakini leo hii ukakuta jamaa huyu anapambana na kazi za ndoto zake….
 
Mara Kila mmoja akawa amebadilika.
 
Na hata lugha ikabadilika. Ukakuta watu hawaongei Tena lugha za kukatishana tamaa. Ukakuta watu wanaongea maneno ya kutiana moyo. Kila mmoja anapenda mafanikio ya mwingine.
 
Dunia hii utakuwa nzuri sana, si ndiyo ee? Bila shaka…
Nakuhakikishia kuanzia siku hiyo, hapa duniania hakutakuwa na vita. Hakutakuwa na marumbano..
Watu hawatajiua wala kuwaua wengine…Naamini wasiwasi kuwa Moja ya kitu kinachofanya watu wajiue ni kwa sababu hawana ndoto, au kama wanazo basi hawazifanyii kazi, au kama wanazifanyia kazi basi wameanza TU kidogo na wamekatishwa tamaa.
 
Lakini hicho nilichokiandika hapo ni kama stori ya Habunwasi. Haliwezi skutokea…
 
Haliwezi kutoka kwa sababu watu wote duniania hawawezi kubadilika ndani ya siku Moja. Wanaohitaji kubadilika kwanza ni mimi na Wewe. Na baadaye watafuata watu wa karibu waliotuzunguka mimi na wewe.
 
Ebu baada ya hapa Anza kujiambia MIMI ndiye ninapaswa kubadilika.
 
Mimi mdiye ninapaswa kuwa na ndoto kubwa. Kuna stori kwenye Biblia kuwa Yesu (Nabii Issa) aliulizwa kuwa marafiki zako ni akina nani? Alisema marafiki zangu ni wale wanaolifuata neno la Mungu na kuliishi…
 
Sasa na Mimi ukiniuliza kutoka moyoni kuwa marafiki zangu ni akina nani?
 
 
Nitakujibu kwa kukwambia kuwa
Marafiki zangu ni wenye ndoto kubwa na ambao wanaziishi hizo ndoto zao.  (kama mpaka Sasa hivi hauna ndoto kubwa, fanya kitu uwe Nayo, ili uendelee kuwa miongoni mwa marafiki zangu.
 
Na njia zuri ya kuigundua ndoto Yako kubwa na kuanza kukifanyia kazi ni kuanza kusoma kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. MARAFIKI zangu wa kweli pia ni wale ambao wamesoma vitabu vyangu na wanajua vinaongelea Nini.
 
Sikiliza, huwezi kukaa unasubiri upewe ruhusa ya kufanyia kazi ndoto yako ukaipata. Kila utakayemshirikisha ndoto yako kubwa atakuwa nay a kwake ya kusema, yupo atakayekwambia kwamba haijawahi kufanyika, mwingine atakwambia kuwa jambo kama hili haliwezekani, mwingine atakwambia kwamba halijawahi kufanyika, mwingine atakwambia kwamba, kama ingekuwa rahisi kila mmoja angekuwa anafanya na mengine…
Ruhusa ya kufanyia kazi ndoto yako kubwa unapaswa kujipa wewe mwenyewe na siyo mwenza wako, serikali, mjomba au mtu yeyote unayemfikiria wewe…
 
Nadhan na mimi naweza kukupa ruhusa pia, ebu  fumba macho kisha jiambie kwamba, kuanzia leo liwe jua au mvua, kiangazi au masika, nitafanyia kazi ndoto zangu…
Kisha toka hapa nenda kafanyie kazi ndoto zako
 
 kwa leo inatosha.

Kuna ofa ya krimasi. Unapata vitabu sita kwa elfu ishirini tu (softcopy)
kama bado hujapata hii ofa changamka. Wasiliana nami kwa 0684408755

Vitabu vilivyo kwenye ofa ni 


1: VYANZO VINGI VYA KIPATO
2: JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA
3: MWONGOZO WA WAPAMBANAJI
4: NGUVU YA KUWEKA MALENGO
5: NGUVU YA WAZO
6: MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA

Ukitaka vitatu kati ya hivyo, utavipata kwa 10,000/- tu.

Kumbuka hii ni ofa ya muda mfupi tu. Ni au unalipia sasa hivi ili kupata hii 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X