Kitu kimoja unachopaswa kufanyia Kazi kwa uhakika 2024


Kitu kimoja unachopaswa kufanyia Kazi kwa uhakika 2024

Rafiki yangu, kuna kitu kimoja ambacho unapaswa kukifanyia kazi kwa uhakika mwaka 2024. Kitu hiki siyo kingine bali ni kutenda kile unachosema.

Usishauri watu kitu ambacho Wewe mwenyewe hutakifanyia kazi.
Usiwaambie watu wafanyevkitu ambacho Wewe hujawahi kufanya Wala mpango wa kufanya. Na Wala hutakaa ukifanye.

Sema kidogo 2024, ila tenda sana
Ukiwaambia watu juu ya habari ya kufanya mazoezi. Kuwa kipaumbele Wewe mwenyewe kwa kufanya mazoezi.

Ukiwaambia watu weka AKIBA. Kuwa kipaumbele mwenyewe kwa KUWEKA AKIBA.

Kumbuka, simaanishi kwamba mwaka huu ujioneshe. Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayejionesha na anayefanya kweli.

Mfano, ninaposema fanya mazoezi. Simaanishi Sasa ujioneshe kuwa unafanya mazoezi. Ukiona mwaka huu unaanza kufanya kitu ili watu wakuone, ACHA.

Fanya kwa msukumo kutoka moyoni na siyo kwa ajili ya kujionesha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X