maeneo matano Unayopaswa kuyawekea NGUVU mwaka 2024 kwenye kusoma na kujifunza na vitabu Unayopaswa kusoma.


Isifike hatua ukaona kwamba umeshajua kila kitu. Siku ambayo utaona umeshajua kila kitu ndiyo siku ambayo utaanza kupoteza. Mara zote kuwa unajifunza.

Kujifunza kuwe sehemu ya maisha Yako. Kama ambavyo Huwa hakuna wakati unaposema sasa nimeshakula inatosha sitakula Tena. Hivyo hivyo, kujifunza. Isifike hatua ambapo utaona kwamba imetosha.

Kila mara kuwa na kitabu unasoma. Jiunge na kozi na programu mbalimbali na jifunze bila kuacha.

Halafu Yale unayojifunza; yafanyie kazi mara zote bila kuacha.

Sijui unanielewa hapo?

Sasa yafuatayo ni maeneo matano Unayopaswa kuyawekea NGUVU mwaka 2024 kwenye kusoma na kujifunza na vitabu Unayopaswa kusoma.

 1. Jifunze zaidi kuhusu PESA. Wengi wanajua kuhusu matumizi ya PESA, lakini hawajui kuhusu kutunza PESA na kuifanya PESA iwafanyie kazi. Mwaka huu jifunze zaidi kuhusu namna ya kuitumikisha PESA. Na itumikishe haswa PESA kuanzia mwaka hata kama ni Kwa kiwango kidogo.

Vitabu Muhimu vya kusoma kwenye hili ni kitabu Cha
👉MAAJABU YA KUWEKA AKIBA 
👉MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE
👉JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA

Anza na hivyo vitabu. Visome vizuri, mwenyewe utafurahi Kwa uamuzi huo utakaokupa umechukua.

 1. Jifunze zaidi kuhusu biashara.
  Ili uweze KUTENGENEZA kipato zaidi unahitaji kujifunza zaidi pia kuhusu biashara. Biashara ni njia ha KUTENGENEZA kipato zaidi ambacho hakina ukomo. Jifunze biashara na fanyia kazi Yale unayojifunza bila ya kurudi nyuma.

Vitabu vya biashara ambavyo unapaswa kusoma 2024 ni pamoja na
👉MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZIAHA BIASHARA
👉NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

Hivi vyote unaweza kuvipata Kwa kuwasiliana na 0684408755 Sasa.

 1. Jifunze kuhusu mtandao na JINSI ya kukutumia kwenye masoko na KUTENGENEZA fedha zaidi.
  Tofauti na zamani ambapo masoko yalikuwa yanafanyika Kwa njia za redio, runinga na magazeti. Leo hii unaweza kuwafikia wengi Kwa simu Yako TU. Unalionaje Hilo. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na maarifa sahihi. Na maarifa haya sahihi utayapata kwenye vitabu hivi.
  👉zama zimebadilika: maisha yamebadilika, ajira hatarini na wewe badilika.
  👉JINSI ya KUTENGENEZA fedha Kwa Kile unachojua.
 2. Jifunze kuhusu KUWEKA MALENGO na kuyafanyia kazi.
  Hili ni eneo unalopaswa kulifahamu hasa Kwa mwezi huu wa Januari.

Vitabu vya kusoma kwenye hili eneo
👉JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO.
👉NGUVU YA KUWEKA MALENGO.

KUPATA vitabu hivyo, wasiliana na 0684408755

 1. Jifunze kuhusu kuongeza kipato chako. Hili litakusaidia mwaka huu kipato chako kisibaki palepale. Kuongeza kipato chako ni Muhimu sana. Maana kipato chako hakipaswi kubaki palepale.

Vitabu Muhimu vya KUSOMA.
👉VYANZO VINGI VYA KIPATO: Usipokuwa na VYANZO VINGI VYA KIPATO, utakuwa na VYANZO VINGI VYA mahangaiko.
👉programu ya ONGEZA KIPATO CHAKO MARA MBILI.

Hayo ndiyo maeneo Muhimu Unayopaswa kuyawekea NGUVU kwenye kujifunza mwaka 2024.

Nikutakie Kila la kheri.

Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X