Vitu 10 Vya Kijinga Ambavyo Unapaswa kufanya Walau Maram Moja Mwaka 2024


Leo nataka nikwambie vitu 10 tu vya kijinga ambavvyo unapaswa kujaribu kufanya walau mara moja ndani ya mwaka 2024

  1. Toa wiki moja ambayo utalala kwa saa tatu, halafu muda mwingine wote unafanya kazi. Fanya hivyo kwa siku mbili mpaka siku sita au wiki na siyo zaidi ya hapo.
  2. Weka akiba mshahara wako wote, halafu tafuta chanzo kingine ambacho kitakufanya ulipie bili na kuendesha maisha yako ya kila siku.
  3. Zima simu wiki nzima, halafu utumie muda huo kujifunza na kufanya kazi
  4. Ifanye siku moja kwa wiki kuwa takatifu kwako. Siku ambayo hutafanya kazi, bali itakuwa ni siku mapumziko na kupangilia ratiba zako za wiki inayofuata.
  5. Siku moja tembea kwa mguu au nenda na baiskeli sehemu ambayo ulikuwa umezoea kwenda kwa gari kama ofisini.
  6. Kwa dakika 15 tu kwa siku weka mziki wowote unaoupenda na cheza kama siyo wewe, kisha endelea na majukumu yako.
  7. Jiwekee utaratibu wa kutoa kitu kila siku hata kama ni kidogo. Kwa kuanzia unaweza kununua mfuko wa pipi, kisha kila siku ukatoa zawadi ya pipi moja kwa mtu yeyote.
  8. Mara moja moja pika chakula mwenyewe. NB. Hii ni kwa wale ambao huwa hawapiki, au wana wapishi au wenza wao wanapika. mara moja moja hasa ile siku unayokuwa umepumzika (rejea namba 4) pika chakula mwenyewe.
  9. Washa moto bila ya kiberiti, wala kuomba kwa jirani. Washa kwa ulimbombo na ulindi
  10. Mara moja lala kwa saa 10 mfululizo

Siyo lazima ufanyie kazi haya yote, fanyia baadhi yale unayoona unaweza kwa sasa. Usiache kuja kutupa mrejesho hapa baada ya kuyafanyia kazi.

Soma Zaidi: Vitu vitano ambavyo hupaswi kuvipoteza kwenye safari yako ya mafanikio

Nakupenda

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

NB: SEMINA YETU YA JANUARI, itafanyika kuanzia tarehe 20-20 Februari

*Karibu kwenye Semina ya Kipekee ya Kufungua Mwaka 2024!*

Rafiki yangu mpendwa,
Karibu kwenye mwaka wa mabadiliko na mafanikio –

Kila mwaka, tumekuwa tukijiwekea lengo la kuleta tofauti katika maisha yetu kupitia semina tatu muhimu.
Ambapo huwa tuna semina ya kufungua mwaka (Januari 15-30)
SEMINA ya ana kwa ana (Jumamosi ya mwisho ya mwezi Juni) na semina nyingine ya mtandaoni (Septemba 24-30)

Kwa Leo ningependa kuongelea
*Semina ya Kufungua Mwaka 2024: Njia Mpya, Matokeo Makubwa!*

Tofauti na miaka iliyopita, semina hii ya Januari itakuwa ya kipekee. Badala ya siku 15, safari yetu ya mabadiliko itadumu kwa mwezi mzima! Kutoka tarehe 20 Januari hadi 20 Februari,

Kwenye hii semina tutajifumza mengi baadhi yakiwa ni pamoja na:

*Siku ya Kwanza: Karibu kwenye semina ya kufanya makubwa kwa vitendo mwaka 2024*

*Siku ya Pili: Anza Leo na Siyo Kesho*

*Siku ya Nne: Jinsi ya kuishinda tabia ya kughairisha*-

*Siku ya Kumi na Mbili: Jinsi simu zinavyoharibu ufanisi wako na nini cha kufanya mwaka 2024*

Mada hizi zote zimeundwa kukuhamasisha na kukusukuma kufikia mafanikio makubwa ndani ya mwaka 2024.

Kila siku itakuletea changamoto mpya na ufahamu wa kipekee. Tutajifunza jinsi ya kujiondoa kwenye tabia zinazotuzuia, kukabiliana na changamoto za kila siku, na kuanza safari ya kujenga mfumo bora wa maisha.

*Ada Yako ya Ushiriki:*

Ada ya semina ni zaidi ya thamani utakayopata – Tsh 30,000/-. Pata nafasi yako sasa kwa kulipa kupitia namba 0684408755 (Godius Rweyongeza).

Hii ni fursa yako ya kuanza mwaka 2024 kwa nguvu mpya na mwongozo wa kufanikiwa.

*Jiunge Nasi:*

Tunakualika kwenye kikundi chetu cha WhatsApp kwa ajili ya semina. Jiunge na wenzako wanaotafuta mabadiliko na mafanikio:

(https://chat.whatsapp.com/CAdCnW82i8N0clD2fDvn7v)

*Fanya Uamuzi wa Kuleta Mabadiliko:*

Hatua ndogo ndiyo mwanzo wa safari kubwa. Hakikisha unathibitisha ushiriki wako mapema na kuwa tayari kubadilisha maisha yako.

Tunakusubiri kwenye Semina ya Kufungua Mwaka 2024  ili uianze safari Yako ya Mabadiliko na Mafanikio!

Karibu sana!

Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X