Vitu vitano ambavyo hakuna mtu yeyote anaweza kufanya Kwa niaba Yako


Vitu vitano ambavyo hakuna mtu yeyote anaweza kufanya Kwa niaba Yako

  1. Hakuna mtu anaweza kukuamini wewe kama unavyojiamini. Wewe ndiye mtu Unayopaswa kujiamini Kwa asilimia zote hata kama wengine hawakuamini. Jiamini. Mwenyewe kwanza

Ukiendelea kujiamini Kwa muda mrefu, hata kama wengine walikuwa hawakuamini, watakuamini TU. Jiamini.

  1. Hakuna mtu anayeweza KUFANYIA KAZI MALENGO Yako Kwa niaba yako. MALENGO Yako, yafanyie kazi wewe mwenyewe Kwa maana hakuna mtu wa kukusaidia kwenye Hilo.
  2. Kuanzisha biashara.
    Kama umekuwa unajiambia kuwa utaanzisha biashara na hujafanya hivyo, fanya hivyo. Hakuna mtu atafanya hili Kwa niaba Yako.
  3. Hakuna mtu atapenda watoto wako, mwenza wako, familia Yako Kwa niaba Yako. Ni jukumu lako
  4. Kufanya mazoezi. Hakuna mtu atafanya mazoezi Kwa niaba Yako.
    Hili jambo sharti ulifanye mwenyewe.

Rafiki yangu, hayo ndiyo mambo matano ambayo hakuna mtu hata mmoja atayaganya Kwa niaba Yako. Unapaswa kuyafanya mwenyewe.

Godius Rweyongeza
+255755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X