Hiki ni kitu muhimu ambacho kitakusaidida kuendelea kuwa na wateja wa kudumu


Rafiki yangu mpendwa, salaam, hongera sana kwa kazi. Siku ya leo nilitaka kukwambia njia moja ya uhakika na ambayo itakufanya wewe uendelee kuwa na wateja wa kudumu kwenye biashara yako. Njia hii siyo nyingine bali ni njia ni kuhakikisha kila wakati unakuwa na mfumo ambao utafuita wateja wapya, unafuatilia wateja wapya na unatoa mafunzo endelevu.

Inawezekana kuna wateja ambao hawajui chochote kuhusu biashara yako, lakini kitendo cha kuwa wanapata mafunzo endelevu, ambapo wanapata kuelimishwa na kuambiwa vitu kadha wa kadha kuhusu biashara yako, kunawafanya waendelee kuifuatilia biashara yako kwa ukaribu. Na kunawajengea hamu ya kutaka kupata bidhaa zako.

Unachotakiwa kufanya siku ya leo, ni kujiuliza ni njia gani ambazo ninaenda kutumia ili kuhakikisha kwamba ninakuwa na mfumo ambao unatafuta wateja kila mara, mfumo ambao unafuatilia wateja kila mara, kutoa mafunzo kwa wateja na kuwageuza mpaka kuwa wateja kamili?

Ukishauweka huu mfumo. Ni wazi kuwa kila mara kutakuwa na mteja ambaye anataka kununua kutokana na mafunzo ambayo atakuwa amepata kutoka kwako.

Karibu sana

Imeandikwa na Godius Rweyongeza. 

Kupata mafunzo zaidi, unaweza kujipatia nakala za vitabu vya Godius Rweyongeza. Wasiliana na Godius Rweyongeza kwa simu; 0684408755

Kupata kozi na programu mbalimbali tulizonazo. Wasiliana nami kwa 0678848396


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X