JINSI YA KUANZISHA MAZUNGUMZO NA MTU YEYOTE


Kuanzisha mazungumzo na mtu hasa yule ambaye hujawahi kuonana naye, huwa ni kitu kigumu miongoni mwa watu. Umewahi kukutana na mtu ukatamani kuongea naye, halafu ukawa unajiuliza utaanzaje, halafu mara kama mlikuwa kwenye basi, yule mtu anashuka nakuondoka na humwoni tena kwenye Maisha yako.

Imewahi kunitokea. Nilikutana na mrembo mmoja kwenye basi, lakini sasa kimbembe kilikuwa ni kwa namna gani naweza kuanzisha mazungumzo na huyu mtu.

Je, nimwamabie kwamba habari, lakni hiyo ingeonekana kama ni salaam ya kawaida. Je, nimwambia nakupenda, ingeonekana nimeenda haraka sana,

Nataka uwe mama wa Watoto wangu, ingeonekana JAMBO LA KITOTO…

Nikakaa kimya, muda ukaenda na baadaye basi likafika mwisho wa safari, akashuka na kuondoka, mpoaka leo hii sijawahi kumwona.

Kitendo cha kuanzisha mazungumzo miongoni mwa watu ni kitu kigumu kidogo. Na leo hii nipo hapa kukupa mbinu za kukusaidia uweze kuanzisha mazungumzo na mtu yeyote, popote pale utakapokuwa duniani.

Unafunguaje mazungumzo na mtu mwingine

Kitu kikubwa ambacho huwa kinawakwamisha watu kuanzisha mazungumzo na mtu mwingine ni namna ya kuanzisha hayo mazungumzo. Hivi kwa mfano, mtu unaanza kumwambiaje, unaongea naye kitu gani cha kufungua mazungumzo.

Hapa kuna vitu vitatu ambavyo unaweza kutumia kwenye kufuyngua mazungumzo na mtu yeyote.

Kwanza unaweza kumwonglea huyo mtu

Pili unaweza kuongelea kuhusiana na hali ya wakati huo

Na tatu unaweza kuongelea kuhusiana nan a wewe mwenywee

Unaweza kuanzisha mazungumzo kwa kuuliza swali. Kwa kutoa wazo lako au unaweza kuongelea kuhusu jambo Fulani ambalo ni ukweli

Unapoanza kuzungumza na mhusika, lengo la kwanza kabisa linakuwa ni kumfanya huyo mtu aoneshe nia ya kuzungumza na wewe. Kumbe mara nyingi njia bora ya kuanzisha mazungumzo ni kwa kuuliza swali ambalo anatakiwa kujibu. Ni njia nzuri ya kuanzisha mazungumzo.

Njia nyingine ya kuanzisha mazungumzo ni kwa kuongelea jambo kuhusiana na hali inayoendelea. Kwa mfano, kama mpo kwenye darasa moja unaweza kuanza kwa kuuliza swali kama; unafikiri ni kitu gani kitakuwepo kwenye mtihani leo..

Au kama mnaenda kwenye usaili; unaweza kuanzisha mazungumzo kwa kumwuliza mtu unafikiri ni kitu gani ambacho wasaili watakuwa wanahitaji kutoka kwetu? Au unafikiri ni maswali gani ambayo yataulizwa..

Kama mmekutana kwenye mechi; unaweza kuanzisha mazungumzo kwa kumwuliza mwenzako kuwa ni unafikiri nani atashinda hii mechi?

Kama mpo sokoni, unaweza kuanza kwa kumwuliza mhusika; naona unanunua nazi; nimekuw anatamani kwa siku nyingi kujua namna ambavyo inapikwa. Unaweza kunipa maelekezo kidogo tafadhali,

Kama ni jirani yako, unaweza hata kuanza kumwambia kuwa naona bustani yako ni ya kijani, nini siri ya kuwa na bustani nzuri kama hii?

Kama nilivyosema mwanzoni. Njia nyingine ya kuanzisha mazungumzo na mtu yeyote ni kwa kuanza kuzungumzia kuhusu huyo mtu. Kwa mfano;

Mtu ambaye amevaa jaketi, unaweza kuanza kwa kumwambia hivi, waoo hongera naona una jaketi zuri kweli, unaweza kunieleza kidogo kuhusu hiyo alama kwenye jaketi inamaanisha nini?

Au labda mmetoka kwenye kikao. Unaweza kuanzisha mazungumzo na mtu kwa kumwambia, yaani umetoa maoni bora kabisa siku ya leo ebu niambie kwa nini…..

Nadhani wengi wanaogopa kuanzisha mazungumzo na polisi au wanajeshi. Unaweza kuanzisha mazungumzo  kwa kumuuliza. Ningependa kujiunga n jeshi la polisi, ni vitu gania mbavyo natakiwa kuzingatia?

Kama mko kwenye sherehe, unaweza kuanzisha mazungumzo kwa kumuuliza mhusika; ni kwa namna gani umefika hapa, yupi ni ndugu yako, bwana harusi au bibi harusi

Kama po mgahwani, unaweza kuanzisha mazungumzo kwa kumwabia mtu kuwa naweza kuungana na wewe kwenye meza tupate chakula kwa pamoja.

Njia ya mwisho kabisa ya kuanzisha mazungumzo ni ya kujiongelea mwenywewe. Ila hii siyo njia bora Zaidi. Maana watu huwa hawapendi watu wanaojiongelea wao wenyewe. Kumbuka kama ambavyo Dale Carnegie anasaema; unapaswa kuonesha kuwajali wengine kuliko unavyojijali wewe mwenywew. Hivyo, unapojiongelea mwenyewe maana yake unakuwa hujaonesha kujali maslahi yao.

Njia bora ya kuanzisha mazungumzo kwa kujiuzungumzia mwenyewe ni kuanza kwa kujitambiulisha. Jitambulishe hivi.

Habari, kwa majina naitwa……………….(JINA LAKO)……………..na wewe jina lako ni……………………………………………….

Hizo ndizo njia unazoweka kutumia kwenye kaunzisha mazungumzo na watu wentgine. Ni njia pi bora kwako ambayo unaenda kutumia siku ya leo. Ebu niambie ni pi ambayo umependa Zaidi.

Ni ipi ambayo unaenda kuitumia…

Ni ipi ambayo huwa unaitumia…..

Tuwekee maoni hapa chini….

Mimi ni Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X