NJIA ZA KUEPUKA KUGHAIRISHA MAMBO 2024


Rafiki yangu mpendwa salaam, hongera sana kwa siku hii nyingine nzuri sana. Leo hii ni tarehe 1.2.2024. ni siku nyingine bora kabisa. Tayari mwezi mmoja umepita tangu tuuanze mwaka mpya wa 2024, kazi imebaki kwako sasa. Ni kwa namna gani mpaka sasa unaendelea kufanyia kazi malengo yako? Unajiona ukiwa unaelekea malengo yako au unakwama sehemu? Kumbuka, mwaka mpya siyo mwaka mpya tena, na usipoanya kitu, maana yake huu mwaka unaenda kuupoteza wote, bila ya kuwa umefanya kitu cha maana.

Kwanza labda nikuulize, una malengo ambayo unayafanyia kazi? Ukweli ni kuwa kama hauna malengo, kuna kosa kubwa ambalo unafanya. Hakikisha kabisa unakaa chini na kuweka malengo yako sasa.

Maandiko mengi ambayo niliandika ndani ya mwezi wa kwanza, yalikuwa yakielekeza namna ya kuweka malengo 2024, namna ya kuyafanyia kazi  hayo malengo na mpaka kuyafikia. Kama kwa bahati mbaya hukufuatila haya mafunzo, nashauri, utembelee blogu yangu ya SONGAMBELE (www.songambele.co.tz) ili uweze kujifunza zaidi kuhusu haya mambo yote ambayo nakwambia.

Nakushauhri pia uweze kujipatia nakala ya kitabu cha NGUVU YA KUWEKA MALENGO. Kitabu hiki ni mwogozo wa kuweka malengo. Kama kwa bahati mbaya mpaka hivi tunavyoingia ndani ya mwezi wa pili, unaingia bila ya kuwa na malengo. Basi, jiwekee mkakati wa kuhakikisha kwamba unakuwa na malengo, mapema sana ndani ya huu mwezi. Malengo ndiyo ramani pekee ambayo itakuongoza, wewe kuelekea na kufikia kule ambapo unataka kufika. Ukweli ni kuwa huwezi kufanikisha mambo makubw kama hauna malengo.

Sasa kwa kuwa tumeshaongelea sana kuhusu malengo, ndani ya huu mwezi wa pili tutakuwa tunaongelea zaidi kuhusu NAMNA GANI AMBAVYO UNAWEZA KUACHA TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO.

Kwa hiyo, ninaenda kuchukulia kwamba tayari una malengo, kama hauna malengo. Pata huo mwongozo ambao nimekuelekeza uupate, ndani ya huu mwezi wa pili nataka uache tabia ya kughairisha malengo na miipango yako ambayo umeiweka kwa ajilil ya mwaka wako 2024. Unaachaje tabia hii tabia.

Sasa tuambatane kila siku kwenye makala ambazo nitakushirikisha karibia kwa mwezi mzima bila ya kuacha.

Kugharisha mambo ni kuacha kufanya jambo ambalo liko mbele yako kwa sasa kwa huku ukiwa unajiambia kwamba jambo hilohilo utalifanya kesho au siku nyingine. Na muda mwingine unaweza kuwa hujiambii kwamba hilo jambo utalifanya kesho au siku nyingine, lakini unaweza kuwa kwenye fikra zako unaamua kwamba unafanya jambo jingine ambalo kwa muda huo unaona kwamba linafaa wakati jambo hilohilo ambalo unafanya siyo la muhimu kwa wkaati huo.

Mfano, jukumu lako kuu kwa wakati huo linaweza kuwa ni kutafuta na kuwafikia wateja kadhaa kwa wakati huo. Lakini ukajikuta kwamba unaacha kufanya hilo jukumu na badala yake unaenda  facebook au kwenye mtandao mwingine wa kijamii na kujikuta kwamba unapoteza muda wako wa thamani huko. Mwisho wa siku uttajikuta unajiambia kwamba hii ndiyo inaenda kuwa ni mara yangu ya mwisho kufanya hili, halafu kesho yake jambo kama hilo hilo linajirudia. Unajuikuta kwamba umerudi kwenye hali hiyohiyo.

Sasa ili tuweze kuachana na tabia ya kughairisha mambo unapaswa kuanza na kuingalia thamani ya muda wkao.

Muda wako ni wa thamani. Najua hili siyo mara yako ya kwanza kuliskikia. Siyo mara yako ya kwanza kusiikia kwamba muda ni mali. Siyo mara yako ya kwanza kusikia kwamba muda unapaswa kuwa unautumia vizuri. Sasa kwa kuwa unajua haya mambo, ninachotaka kukwambia ni kukueleza kwa undani zaidi ni kwa namna gani muda ni wa thamani..

Hivi inakuwaje muda unasemwa kuwa na thamani kiasi hicho. Yaani, muda unakuwaje mali? Hili limeanzaje?

Ngoja nikuelekeze vizuri ili uweze kunielewa.

Mimi, wewe na mtu yeyote unayemfahamu leo hiii hapa duniani, na hata wale usiowafahamu, sote kwa siku moja tuna saa 24. Hakuna mtu yeyote Yule ambaye ana muda mwingi zaidi ya mwingine. Mpaka leo hii unaposoma hapa, hakuna kifaa chochote kile ambacho kimegunduliwa ambacho kinaweza muda wa mtu yeyote.

Sekunde moja ambayo imepita sasa hivi, naam, hii sekunde, haitakaa irudi tena. Ikishapita ndiyo itakuwa imepita, ni juu yako sasa kuhakikisha kwamba kila sekunde inayokuja kwako unaitumia vyema kabisa.

Moja ya kipengele muhimu sana linapokuja suala zima la muda ni kwmaba muda huwezi kuukopa, wala kuukopesha. Muda siyo kama fedha. Na ndiyo maana unaambiiwa kila siku kuwa unaweza kukopa fedha, lakini huwezi kukopa muda. Limekaaje hili, ngoja nikuoneshe hapa..

Tuanze na dhana ya kukopa na kukopesha fedha. Leo hii ukiwa hauna fedha, unaweza kwenda benki yoyote ile na kuwaambia kuwa ungependa kukopa kiasi fulani cha fedha, halafu hiyo benki, watakuwa tayari kutoa fedha na kukupa. Lakini huwezi kwenda benki kukopa muda.

Leo ikitokea kwamba una fedha nyingi, unaweza kuwakopa rafiki zako. Au unaweza kuwekeza hizo fedha sehemu yoyote ile ambayo unataka wewe. Lakini ukweli ni kuwa huwezi kukopesha muda wako kwa mtu. Akautumia muda wako halafu akaja kukurudishia muda wako baadaye.

Ndiyo maana tunapoanza kuliangalia suala zima la kughairisha mambo tunapaswa kuanza kuliangalia suala la muda wako. Maana vitu vyote tunavyovifanya kuelekea malengo yetu, na vitu vyote ambavyo hatufanyi, yote hayo tunayafanya ndani ya muda tulionao.

Sasa swali langu la kwanza kwako ni kuwa muda wako una thamani kiasi gani?

Njia rahisi ya kutambua thamani ya muda wako nia kuangalia kipato ambacho unaingiza sasa hivi

Kama kwa sasa hivi unaingiza kipato cha milioni  moja kwa mwezi. Maana yake thamani ya saa lako moja ni milioni moja kugawa kwa siku thelathini, kugawa kwa saa 24. Yaani, (1,000,000/30/24) tunapata kuwa thamani ya saa lako moja ni sawa na 1,388.88

Huwa napenda kuipima thamani ya muda wako kwa kuangalia zaidi kile kipato ambacho ungependa kufikia ndani ya huu mwaka.

Kama huu mwaka ungependa kipato chako kiwe ni milioni mbili. Maana yake ni kwamba milioni 2,000,000/30/24. Maana yake thamani ya ya muda wako ni 2,777.77

Ila ngoja ni kwambie kitu, kama umepiga kwa kutumia hizi hesabu na bado thamani ya muda wako ni chini ya elfu tano, sikiliza, weka kiwango cha chini kabisa cha thamani ya saa lako moja kuwa elfu tano. Hiki ndicho kinapaswakuwa kiwango chako cha chni kabisa kwa mtu wa nguvu kama wewe ambaye unafuatilia mafunzo yangu kila mara, ni kiwango amabcho unapaswakuanza kukifnayia kazi.

Hii ndiyo kusema kwamba haupaswi kufanya kitu chochote ambacho ni cha viwango cha chini ya elfu tano kwa saa yako moja.

Kama kitu unachofanya ndani ya muda wako ni cha thamani ya chini. Yaani, thamani yake ni chini elfu tano kwa muda huo. Ujue kwamba unajiumiza.

Kwa kulijua hili litakusaidia wewe kuweza kujali muda wako zaidi na kuwekeza muda wako kwenye maeneo ambayo yanazalisha matokeo makubwa zaidi kuliko eneo jingine.

sasaa baada ya kujua thamani ya muda wako, maana yake hii itakuongezea hasira ya kujali zaidi muda wako kuliko mtu mwingine yeyote.

Lakini pia hutakubali kufanya majukumu ambayo yapo chini ya viwango vyako

Sasa mtu mmoja aliniuliza, kuwa kama thamani ya muda ni elfu tano kwa saa. Lakini kuna saa ambazo ninakuwa sipo kazini, ambao ni muda kaupumzika.

Ngoja nikwambie kitu.

Muda wako unapaswa kuwa na thamani bila ya kujali ndani ya huo muda unafanya kazi au hufanyi kazi.

Muda wakowote unapaswa kuwa na thamani, ngoja nikuelekeze zaidi.

Namna unavyotumia muda wako wa ziada, muda wako wa mapumziko, ndivyo ambavyo utaweza kutumia muda wako wa kazi. Kama muda wako wa mapumziko unalewa, kwa kisingizio kuwa ni muda wako wa mapumziko. Ni ukweli kuwa huwezi kuzalisha matokeo muda wa kazi ukifika na huwezi kuwa na ufanisi.

Jambo  hili litapekelea wewe kuwa ufanisi kidogo na kuzalishaji kidogo muda wa kazi. Kumbe, kwa sababu hiyo, unapaswa kuheshimu muda ambao hufanyi kazi, kama ambavyo unaheshimu muda wako wa kufanya kazi. Unapaswa kuheshimu muda wako wa kulala kama amabvyo unaheshimu muda wako mwingine. Kwa sababu hivi vitu vyote vinaungana, namna unavyotumia muda wako mwingine wa mapumziko, ndivyo ambavyo utatumia muda wako wa kazi. Ukitumia muda wako wa ziada, muda wa kazi pia hutaweza kuzalisha matokeo mazuri na yanayoeleweka.

Sasa kazi ambayounapaswa kufanya siku ya leo ni moja hasa tunapoanza kuliongelea zaidi suala zima la kughairisha mambo. Jua thamani ya muda wako. Kama bado hujui thamani ya muda wako, yaani ksa saa moja, weka kiwango cha chini kabisa kuwa elfu tano, unawez akuweka kiwango chochote kile cha juu, ila isiwe chini ya elfu tano.

Je, wewe umeifahamu thamani yako ya muda?

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza; kupitia mtandao wake wa songambele (www.songambele.co.tz)

Kwenye mitandao ya kijamii. Godius Rweyongeza apatikana kama Godius Rweyongeza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X