Fedha ina kanuni zake ambazo unapaswa kuzifahamu na kuzitumia vizuri. Moja ya kanuni hii ni kanuni ya rasilimali na dhima. Hiii ni muhimu sana kwako eafiki yangu kifahamu ili usije ukaingia kwenye mtego.
Kulingana na kanuni hii ni kwamba unapaswa kununua zaidi rasilimali (assets) kwa sababu hizi rasilimali ndizo zinakuingizia fedha mfukoni kuliko unavyonunua dhima (liabilities).
Kabla ya kununua kitu chochote jiulize hivi je, hiki ni rasilimali (asset) au dhima (liability) kama kinatoa fedha mfukoni basi jua wazi kuwa hiyo ni dhima.
Kazi yako ya kwanza inakuwa ni wewe kuhakikisha kwamba unawekeza kwenye rasilimali zaidi.
Inashauriwa kama unataka kununua dhima, utafute fedha mara mbili zaidi na uiwekeze kwenye rasilimali. Kwa mfano kama unataka kununua gari, jiulize naweza kununua mawili. Kama huwezi kununua magari mawili, maana yake unapaswa kuweka juhudi zaidi ili upate fedha ya kununua magari mawili kwanza ambayo umeiwekeza, kisha sas andiyo ununue gari yako.
SOMA ZAIDI: Sheria Muhimu Katika Kutengeneza Pesa Na Kuwa Tajiri
Kwa leo inatosha au unasemaje.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755
For Consultation only: +255 755 848 391