MAAJABU! Hii Ndiyo Siri Usiyoijua Kuhusu Watu Waliofanikiwa


Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Nina uhakika leo inaenda kuwa ni moja ya siku yako bora kabisa

Moja ya kitu ambacho watu wengi wamekuwa hawafahamu ni siri kutoka kwa watu waliofanikiwa. Wengi hudhani kuwa hawa watu waliofanikiwa, basi wamekuwa hivyo aidha kwa kuzaliwa, au walikutana na bahati tu hapa njiani.

Hiki kitu kimekuwa kinawasukuma wengi kutafuta njia za mkato za kutafuta mafanikio. Ila ukweli ni kuwa hakuna njia za mkato, ambazo unaweza kutumia ili kufikia mafanikio makubwa, na mara nyingi, njia za mkato ndizo huwa ni njia mbaya zaidi.

Ni njia mbaya zaidi kwa sababu, kwa sababu zinakufanya unapoteza siyo tu muda, bali rasilimali pia. Njia za mkato ndiyo njia ndefu zaidi kwenye kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa.

SOMA ZAIDI: Njia PEKEE Ya Mkato Itakayokupa Mafanikio Makubwa Ni Hii Tu

Kitu pekee ambacho unapaswa kujua kuhusu watu waliofanikiwa ni kwamba hawa watu siyo kwamba wamefanikiwa ndani ya siku moja tu. Hapana.  Hawa watu wamekuwa wanafanya kitu kimoja kwa muda mrefu.

Kitu kimoja unachopaswa kufahamu, kabla hujakata tamaa, kabla hujaona kwamba hiki ninachokifanya hakiwezekani. Kitu kimoja unachopaswa kufahamu ni kuwa unapaswa kuendelea kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa kwa muda mrefu bila ya kuacha.

Kama kitu unachokifanya hujakifanya kwa bidii zako kwa miaka zaidi ya mitano, basi jua wazi kuwa unapaswa kuendelea kupambania malengo na ndoto zako kubwa mara zote.

Rafiki yangu, nadhani kwa leo inatosha. tukutane kesho kwa makala nyingine bora kabisa kama hii.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755

For Consultation only: +255 755 848 391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X