Hii Ndiyo Gharama Halisi Unayopaswa Kulipa Ili Kufanikiwa Kwenye Biashara


Nyuma ya ushindi wa biashara kuna vitu ambavyo unapaswa kufanya ili uweze kuisogeza biashara yako mbele. Baadhiya hivi vitu vinahitaji ujitoe, kuliko mtu yeyote.

 

#1. Kuchelewa kulala, hii mojawapo ya gharama ambazo unapaswa kulipa kama mfanya biashara katika kujenga biashar ayako. Kuna nyakati nyingi ambazo utahitaji kutumia muda mwingi kazini kwa ajili ya kukamilisha jambo fulani ambalo liko mbele yako. Kuwa tayari kulipa gharama hii pale itakapohitajika

 

#2. kuamka mapema

mmbali na kuwa utapaswa kulala umechelewa, kuna nyakati utakuwa wa mwisho kulala na wa kwanza kuamka. Yaani, hapo umelela saa sita au saa saba, na saa kumi kamiili alfajiri upo macho na kazi inaendela. Kuwa tayari kw aajili ya hili, ila kama hujaanza biashara usiogope.

 

#3. Kuweekeza katika wewe

Hi ini gharama nyingine muhimu sana ambayo unapaswa kuilipa. Ukweli ni kuwa biashara itakuwa kulingana na vile uyakavyokuwa unakua wewe. Kama wewe hukui, biashara haitakua pia.

kama wewe unadorora vile vile biashara itadorora.

 

#4. KUWEKEZA pesa

Hiki ni kitu kingine muhimu ambacho kama mfanyabishara utapaswa kukifanya. Unahitaji kuwkeza fedha zako. Kuna maeneo muhimu ambayo mfanyabishara yeyote makini anapaswa kuwekeza fedha zake.

Eneo la kwaza ni kuwekeza fedha kwenye biashara yako. Hili ni eneo la kwanza kabisa ambalo unapaswa kuwekeza fedha zako kama mfanyabiashara.

Eneo la pili ambapo unapaswa kuwekeza fedha zako ni kwenye hisa, hatifungani na vipande kupitia soko la hisa la Dar Es Salaam

Na eneo la tatu ni kuwekeza kwenye elimu na kujifunza.

 

Hayo ndiiyo maeneo ambayo kama  mfanyabiashara unapaswa kuwekeza fedha zkao.

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X