Rafiki yangu wa ukweli, bila shaka unaendelea vyema kabisa na shughuli zako za kila siku.
Siku ya leo nimekuandalia makala ya kushangaza kidogo. Na makala hii ni utabiri.
Mimi syo mtu ninayeamini sana kwenye tabiri, unabii na vitu vinavyoendana na hili.
Ila leo nimevutwa kukupa utabiri huu, na ninatoa utabiri huu nikiwa na uhakika kuwa lazima huu utabiri utatokea kwenye maisha yako. Nina uhakika kabisa wa asilimia 100.
Utabiri wangu unasema kwamba huwezi kufikia malengo ambayo hujaweka. Rafiki yangu, tuwe tu wakweli, kama hujaweka malengo, kama hauna malengo ambayo unapaswa kufikia ni wazi kuwa huwezi kufikia malengo hayo.
Kiufupi ni kuwa huwezi kufikia malengo ya kitu ambacho wewe mwenyewe hauna.
Hivyo, njia bora ya wewe kufikia malengo yako ni kuanza kuweka hayo malengo sahihi kwanza.
Kisha kuanza kuyafanyia kazi.
Nje na hapo tusidanganyane, hutaweza kufanikisha na kufikia hayo malengo ambayo wewe mwenyewe hauna.
Hivyo, kazi yako kubwa ambayo unapaswa kuifanya siku ya leo ni kuhakikisha kwamba umeweka malengo. Weka malengo ambayo utaanza kuyafanyia kazi mara moja kuanzia leo hii.
Ni hivyo tu.
Uwe na siku njema sana rafiki yangu.
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli.
SOMA ZAIDI: NGUVU YA KUWEKA MALENGO