App hii hakikisha unaiweka kwenye simu yako, tena iweke sasa hivi


 

Mara kwa mara huwa nikikutana na app ambayo ni nzuri, basi huwa siachi kukushirikisha na wewe ili uweze kunufaika na kile kilichomo kwenye app husika. Nimekuwa nikifanya hivyo hapa mara kwa mara.

Siku kadhaa zilizopita nilikutana na app inayoitwa the secrets of the billionaires mind, niliipakua na kuiweka kwenye simu yangu. Kiukweli imekuwa ni moja ya app bora kabisa ambazo na wewe unapaswa kuwa nazo.

App hii ni kitabu. INAELEKEZA HATUA KWA HATUA NAMNA UNAVYOWEZA kuwa na fikra za kibilionea.

Mwandaaji wa hii app amejikita zaidi katika kubadili namna unavyofikiri.

Badala ya kufikiri katika namna ya ukawaida, uanze kufikiri kama bilionea.

Ni fikra zetu ndizo zinatufanya kuwa tulivyo.

Hii ndiyo kusema kwamba kama tunataka kubadili matokeo tunayopata sasa hivi, tunapaswa pia kuwa tayari kubadili namna yetu ya kufikiri ya sasa hivi.

Sura zilizo kwenye hiki kitabu hazijazungumzia zaidi kuhusu pesa.

Lakini ni ukwlei kuwa ukiweza kuwa na fikra za kibilionea kama hizo ambazo mwandishi ameeleza kwenye hii app. Na kama matendo yako yatakuwa ya kibilionea, ni wazi tu kuwa suala la kuufikia ubilionea litakuwa ni suala la muda tu.

 

Utaweza kuufikia ubilionea bila ya shida yoyote.

 

Hakikisha unapakua app yako sasa hivi, naamini baada ya kuwa umesoma kilichomo, utarudi hapa na kutoa mrejesho wako binafsi.

 

Makala hii imeandadaliwa na rafiki yako wa ukweli

Godius Rweyongeza

Tuwasiliane kwa namba ya simu 0684408755


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X