Na kosa hili ni wewe kuweka fedha yako sehemu moja tu.
Hili ni kosa kubwa sana kwa sababu ukiwekeza fedha yako sehemu moja na sehemu hiyo ikipata shida, utakuwa umepata shida pia.
Kwa hiyo, badala ya wewe kuweka fedha zako sehemu moja unapaswa kuwa na maeneo kadha wa kadha ya kuweka fedha zako.
na hivyo kuugawa utajiri wako kwa usawa. Kwa leo tunaenda kutumia kanuni ya 25/4 Kulingana na kanuni hii ni kwamba asilimia 25 ya fedha zako zinapaswa kuwa keshi.
Asilimia 25 ya pili ya fedha zako inapaswa kuwa maeneo ambapo ukikimbilia unaweza kuipata haraka kama benki, kwenye fixed deposit au kwenye uwekezaji wa vipande ambapo zinaweza kupatikana kwa haraka.
Asilimia 25 ya tatu inapaswa kuwa kwenye uwekezaji wa hisa Asilimia 25 ya mwisho kwenye mali zisizohamishika kama mashamba na nyumba.