Mtoto Ni Urithi Wako


Kwa kitabu “1,000 YENYE NGUVU”Mwandishi : Jegi Bassu

Mwandishi huyu kwa kitabu hiki kutoka sura ya kwanza hadi mwisho anaendelea kutupa masomo muhimu sana kuhusiana na urithi wa mali tutazoacha duniani wakati ambapo tutaaga hii dunia.

Akitoa nukuu mbalimbali kutoka Baiblia takatifu anatufundisha waziwazi kwamba:

1.Urithi wetu kama wazazi nambari moja ni watoto. Kwa hivyo basi, wazazi tunapaswa kuwaanda hawa warithi vyema katika nyanja mbalimbali kielimu, kiafya, kifedha, kibiashara, kimaadili n.k ili kazi zao zote na mali wanakusanya leo na siku zambeleni haitapotea bure.

2. Aligusa jambo la kutowajua watoto wetu kuwa nani siku za mbeleni. Akanukuu pia kutoka bablia takatifu kuwa mtoto ni zawadi au thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye yeye ndio anamfahamu kwa makusudi huyo mtoto alizaliwa na atafanya nini.

Mwandishi anaendelea kuwambia wazazi kwamba hawachukulie watoto wao kama kawaida au kuwadharau ila wajue kwamba watoto hawa kwa mtazamo wa Mungu watafanya makubwa, huwa na vyewo na mamlaka japo wakati wao ku’angaa nakujitambulisha kwa dunia nzima haijafika.

Nukuu kutoka Biblia takatifu kuhusu Daudi baado alikuwa mchanga na baado hajakuwa mfalme wa ISRAELI nzima:

1 samueli 16:10 1 mambo ya nyakati 29:263.

Mwanao ni balozi mpambanaji wakati mwanao akipambania maisha yake mwanzoni kama akiwa shuleni, vilevile anafanya kwa bidii na kuwakilisha wazazi, familia, jamii na mahali alipotoka kama balozi na kamwe hauwezi kuwaangusha.

Mwandishi anatueleza wazi kabisa kuwa mwanao akiwa shule mbali na pale alipozaliwa au alipokulia, hawezi tena kufikiria mawazo ya kijijini bali anajenga malengo makubwa ya kufika mbali kimaendeleo.

4. kujitengenezea “CONNECTION” Sambamba na kupata hamasa akiwa mbali na nyumbani kwao, mwanao anapofunza shule anajijengea mahusiano, udugu na marafiki na wale wenzake kutoka sehemu mbalimbali za nchi husika ili kumsaidia siku za mbeleni atapopambania riziki yake.

Mwandishi alisisitiza kuwa ofisi au mahali ambapo atapokwenda siku a mbeleni atawakuta wenzake walisoma naye darasani na jambo lolote lite litakuwa mezani au litalomsumbua, litatatulia kwa urahisi sana na marafiki wake wa shule walizosomea pamoja.

5. Mwandishi anatuambia kama wazazi kwamba kamwe tusipojiambia kitu fulani ” HAIWEZEKANI” kwa ajili ya kumtayarisha mwanao na kumkabidhi kuwa urithi wako badala yake tujiulize hivi jambo fulani hili ”

LITAWEZEKANAJE?”Kama tunajiuliza litawezekanaje, basi akili yetu itaanza kuwaza na kujipangilia namna ya kuyaleta shuluhiso za kuondoa hilo tatizo au changamoto na kulifanyia kazi.

6. Mwandishi aligundua siri kubwa inawazuia baadhi ya wazazi kutowezesha watoto wao kupata elimu bora ili iwawezeshe watoto kujimudu na kujipambania vyemu dunia, ni gharama kubwa za ada za shule bora.

Japo kuna hio changamoto ya ada, lakini anatoa baadhi ya mipangilio na biashara mbalimbali ukiwemo zile za kuwekeza kwa muda mrefu wakati mtoto anapokuwa mchanga na hatimaye huo wekezaji hutaweza kumnusuru mzazi na kulipa ada ya mtoto kwa urahisi sana wakati atakapoanza shule.

Mwandishi wa makala hii ni Dkt. Amos Busingye

Ambaye ni daktari wa binadamu na mwanzilishi wa Zahanati ya Busingye Clinic iliyo nchini Uganda, unaweza kutembelea blogu yake kupitia


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X